Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Karagwe Godwin M. Kitonka akitangaza matokeo ya uchaguzi wa kiti cha Ubunge wa jimbo la Karagwe ambapo amemtangaza Mgombea ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa kuwa mshindi wa Ubunge jimbo la Karagwe katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020. Karagwe, Kagera.
Aliyekuwa Mgombea ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa(kushoto) akionesha hati ya kuchaguliwa kuwa mshindi wa Uchaguzi wa jimbo la Karagwe baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Karagwe Godwin M. Kitonka kumtangaza Mgombea ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa kuwa mshindi wa Ubunge jimbo la Karagwe katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020. Karagwe, Kagera.
Aliyekuwa Mgombea ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa akiongea na wananchi waliojitokeza kusikiliza matokeo ya uchaguzi baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Karagwe Godwin M. Kitonka kumtangaza Mgombea ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa kuwa mshindi wa Ubunge jimbo la Karagwe katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020. Karagwe, Kagera.
…………………………………………………………………………………
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Karagwe Godwin M. Kitonka amemtangaza Mgombea ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa kuwa mshindi wa Ubunge jimbo la Karagwe katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020 wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani . Karagwe, Kagera. Oktoba 30, 2020.
Jimbo la Uchaguzi Wilaya ya Karagwe lilikuwa na Wagombea wawili kwa nafasi za ubunge ambao ni Ndugu Innocent Lugha Bashungwa kutoka Chama Cha Mapinduzi na Ndugu Adolf Peleus Mkono kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
Jumla ya kura zilizizopigwa ni 85,922, kura zilizoharibika ni 1,788, Kura halali ni 84,144. Ndugu Adolf Peleus Mkono kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amepata Kura 15,773 ambayo ni sawa na 18.35% ya kura halali na Ndugu Innocent Lugha Bashungwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) amepata kura 68,371 ambayo ni sawa na asilimia 81.254 ya kura halali.