*************
6 JULAI, 2019
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amefanya ziara kwenye mradi wa maji wa pamoja unaohusisha Halmashauri Tatu za Msalala, Nyang’hwale na Shinyanga Vijijini maarufu kama Joint Water Partnership Project (JWPP) kwa lengo la kujionea hatua iliyofikiwa ya utekelezwaji wake.
Mradi huo utanufaisha zaidi ya wananchi 100,000 kutoka vijiji 14 ambavyo ni Mhando, Mwenge (Halmashauri ya Shinyanga vijijini), Nyugwa, Mwamakiliga, Izunya, Karumwa, Kafita, Lushimba (Nyang’hwale) na Kakola Namba 9, Rwabakanga, Busindi, Bugarama, Bushing’we, Ilogi (Msalala).
Katika ziara hiyo, Waziri Mbarawa aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamkala ya Maji Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga ambao ndio wasimamizi wa mradi.