*****************************************
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Hai amemtangaza Shaashisha Mafuwe wa CCM kuwa Mshindi wa Ubunge Jimbo la Hai kwa ushindi wa kura 89,786 huku nafasi ya pili ikiwa imechukuliwa na Freeman Mbowe (CHADEMA) mwenye kura 27,684 na wa tatu ni Mbaruku Mhina (ACT) mwenye kura 315.
Kiongozi huyo wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ambaye alidumu kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu sasa wanaanchi wameamua kufanya mabadiliko na kuamua kumchagua Shaashisha Mafuwe kuliongoza jimbo hilo kwa miaka mitano ijayo.