***************
NA EMMANUEL MBATILO
Kumekuwa na wavuvi waakipata shida hasa katika manunuzi ya samaki hivyo kuna daktari amefanya utafiti na kuja na teknolojia ya mtambo utakaoweza kukausha dagaa tani moja kwa nusu saa ambayo itakuwa ni fursa akisambaza teknolojia hiyo.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi msaidizi Huduma za Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw.Antony Dadu katika Mkutano wa Ana kwa Ana ya Biashara (B2B Metting) katika Maonesho ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wafanyabiashara, Wafugaji na Wakulima mbalimbali, Bw. Dadu amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele kuchangamkia fursa katika sekta ya Uvuvi kwani imekuwa na faida kubwa kwa kutengeneza kipato kitakachokusaidia kuinuka kiuchumi.
“Tunahamasisha watu waweze kujiunga katika uvuvi kwenye bahari kuu ili kumuwezesha kupata kipato kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi. Jaribuni kutengeneza teknolojia ambayo itakuwa inafaida katika sekta ya Uvuvi ili kuweza kukufanya unufaike, gereji za meli hapa Tanzania hakuna mpaka Mombasa ndo ipo hivyo jaribuni kutengeneza teknolojia mbayo ityaweza kufanya hivyo”. Amesema Bw. Dadu.
Aidha Bw. Dadu ameongeza kuwa Ufugaji wa Samaki kwenye vizimba unaweza kukusaidia kupata kipato kikubwa na ukawa mfanyabiashara mkubwa katika huuzaji wa samaki.