……………………………………………………………………………..
01. “Uzushi unaweza ukaongezeka, ulaghai unaweza ukaongezeka kadri tunavyoelekea mwisho wa kampeni, Maelekezo ya Mwenyekiti na Mgombea wetu wa Urais Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, tuendelee kuwa na uvumilivu.”
02. “Mpaka sasa kuna matusi makubwa manne yaliyoporomoshwa dhidi ya mgombea wetu, mgombea wetu kaitwa mwizi na jambazi, kichaa na mwenda wazimu, ipo kwenye rekodi tumevumilia, siku zilizobaki tuongeze uvumilivu, kiongozi wetu kaitwa jalala na kinyago kilichochongwa na kinachostahili kuchomwa, tumevumilia, tuongeze kiwango cha uvulivu.”
03. “Maelekezo ya Mwenyekiti na Mgombea wetu wa Urais Mhe. Dkt. Magufuli, mpaka tarehe 24 Oktoba tunakwenda vizuri na tunatii sheria za uchaguzi, anawaomba mpaka tarehe 27 siku ya mwisho ya Kampeni, tujitahidi tumalize kwa heshima, nawaomba kamati za ushindi, kampeni zifungwe mapema, zisivuke saa tisa alasiri.”
04. “Tunao madiwani zaidi 4000 na wabunge zaidi ya 200, wakiwepo wale waliopita bila kupingwa, wote wanaelekezwa na Mwenyekiti wetu na Mgombea wa Urais Dkt. Magufuli, waendelee na kampeni mpaka tarehe 27 saa tisa alasiri, saa kumi alasiri Mwenyekiti wetu na Mgombea wetu atakuwa anahutubia wananchi kupitia vyombo vya habari akiwa Dodoma na hotuba hiyo itakuwa mubashara vyombo vyote vya habari.”