Muwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Afisa Tarafa ya Zuzu,Lucas Mbise,akizungumza na waumini wa Kanisa la Uweza wa Bwana Tanzania wakati wa maombi maalum kwa ajili ya kuliombea Taifa kufanya uchaguzi kwa Amani Ibada hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya waumini wa Kanisa la Uweza wa Bwana Tanzania wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Dodoma aliyewakilishwa na Afisa Tarafa ya Zuzu Bw.Lucas Mbise wakati wa maombi maalum ya kuliombea Taifa kufanya uchaguzi kwa Amani,Ibada hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Askofu wa Kanisa la Uweza wa Bwana Tanzania Amos Mapigano ,akiongoza maombi maalum pamoja na viongozi wa Serikali kuliombea Taifa kufanya uchaguzi kwa Amani,Ibada hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Waumini wa Kanisa la Uweza wa Bwana Tanzania wakiwa katika Maombi maalum ya kuliombea Taifa kufanya uchaguzi kwa Amani,Ibada hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Askofu wa Kanisa la Uweza wa Bwana Tanzania Amos Mapigano akiwa na viongozi wake wakati wa maombi maalum ya kuliombea Taifa kufanya uchaguzi kwa Amani.
Wanakwaya wa Kanisa la Uweza wa Bwana Tanzania wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya kuliombea Taifa kufanya uchaguzi kwa Amani Ibada hiyo imefanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kanisa la Uweza wa Bwana Tanzania, Jijini Dodoma, limefanya maombi maalum ya kuombea Taifa kufanya uchaguzi kwa amani.
Akizungumza kwenye maombi hayo,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma aliyewakilishwa na Afisa Tarafa ya Zuzu Bw.Lucas Mbise amesema kuwa watanzania kutokubali kushawishiwa au kuonesha viashiria vya uvunjifu wa amani na kuwakataa watu ambao hawaoni maana ya amani iliyopo.
”Kwanza nawapongeza viongozi wa Kanisa la Uweza wa Bwana Tanzania kwa kubuni wazo hilo la kujumuika na waumini wenu kwa kutualika sisi viongozi wa Serikali kwa ajili ya maombi maalum kwa kuliombea Taifa letu kuelekea katika uchaguzi ili uwe na Amani hivyo ni wajibu wetu kulinda Amani”amesema Mbise.
Hivyo ni vyema viongozi wa dini kuweka pembeni ushabiki wa vyama na kutimiza wajibu wenu wa kuhakikisha mnahamasisha waumini wenu kulinda amani.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Uweza wa Bwana Tanzania Amos Mapigano,amesema kuwa hakuna aliyebora kuliko amani ya Tanzania hivyo ni wakati mzuri wa kushika kwa maombi ili tufanye uchaguzi kwa amani.
“Tuendelee kuiombea nchi yetu,tuendelee kulinda amani iliyopo katika Nchi yetu sisi Kanisa la Uweza wa bwana tunawasihi watanzania kuendelea kulinda amani iliyopo kwa nguvu zote hasa kipindi hichi cha uchaguzi,”amesema Mapigano
Awali akisoma waraka wa Kanisa hilo,Katibu wa Kanisa hilo,Boniface Kisinga amesema kuwa wagombea wote katika nafasi za ubunge,udiwani na urais wanatakiwa kukubali matokeo na wasiweke ubinafsi kwani kipaumbele ni kuendelea kuilinda amani ya nchi.
“Tunatoa rai kwa wagombea wote katika uchaguzi mkuu wakubali matokeo na kuondoa ubinafsi wa kukataa matokeo,”amesema Kisinga.
Kisinga maesema kuwa kipaumbele cha kwanza cha watanzania ni amani hivyo watanzania wana wajibu wa kuilinda kwa nguvu zote wakati huu nchi ikielekea katika uchaguzi mkuu.
Katibu huyo aliwataka watanzania kutokubali kushawishika kuivunja amani iliyopo katika kipindi hichi cha uchaguzi.
“Shida yoyote ikitokea tutapata shida, kupoteza amani ni kujipoteza sisi wenyewe kwahiyo tunatoa rai kwa Watanzania tusikubali kushawishiwa kwa namna yoyote ile ya kuonesha viashiria vya uvunjifu wa amani
“Kwa pamoja tuwakatae watu ambao hawaoni umuhimu wa amani madhara ya kupoteza amani ni makubwa kwani chuki na vifo kila mahali kwani kila Mtanzania anawajibika kulinda amani maana ndio mboni ya watanzania,”amesisitiza
Aidha amesema kuwa Kanisa la uweza wa bwana linatoa rai kwa Mamlaka zinazohusika na ulinzi wa Nchi wasiogope kuwashughulikia watu wanaotaka kuvuruga amani hivyo na kwamba hawataki kuona nchi inakuwa na vurugu.
“Tunatoa rai kwa viongozi wa dini na misikiti na makanisa wawaambie waumini na kuwaonya wasiwe sehemu ya kupoteza amani bali tuhamasishe kushiriki kupiga kura.
“Tukishikamana pamoja tutavuka pamoja na uchaguzi utapita na wote tutaendelea kuwa salama hivyo kila Mtanzania amwambie Mtanzania mwenzake tumeridhika na Tanzania yetu hatutaki machafuko,”amesema