Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akiongoza Brass Band ya polisi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Safari za treni kutoka Dar es salaam, Tanga na Arusha unaofanyika leo Jumamosi Oktoba 24, 2020 hi jijini Arusha ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk. John Pombe Magufuli kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
Brass Band ya Polisi ikitumbuiza katika hafla hiyo inayofanyika jijini Arusha ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli atazindua safari za treni Kati ya Dar es salaam, Tanga na Arusha.
Wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro Anna Mghwira, Martine Shigella Tanga na Joseph Mkirikiti Manyara wakiwatunza wanamuziki wa Brass Band ya Polisi wakati wakitumuiza katika hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Ndugu Kenani Kihongosi akiimba wimba maalum aliomtungia Rais Dk. John Pombe Magufuli katika uzinduzi wa Safari ya treni ya TRC Kati ya Dar es salaam , Tanga na Arusha leo jijini Arusha.
Viongozi mbalimbali wa dini wamehudhuria katika hafla hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mama Anna Mghwira na Mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika hafla hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wakiwa katika hafla hiyo.