Katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel akizungumza na wakaguzi wa chakula cha mifugo(hawapo pichani) wakati akifunga semina yasiku mbili kwa wakaguzi hao mkoani morogoro
Mkurugenzi wa uendeshaji wa malisho na vyakula vya mifugo Dk Asimwe Rwiguza akizungumza na waandishi wa nje ya semina ya wakaguzi wa chakula cha Mifugo Mkoani Morogoro.
Katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole(aliyevaa suti nyeusi na miwani)kushoto ni Mkurugenzi wa uendeshaji wa malisho na vyakula vya mifugo Dk Asimwe Rwiguza wakiwa katika Picha ya pamoja na wakaguzi wa chakula cha mifugo kutoka kanda ya mashariki.
wakaguzi wa chakula cha mifugo wakipata ufafanuzi kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kiwanda cha kuzalisha chakula cha mifugo cha International Tanfeeds Ltd kilichopo Mkoani Morogoro,walipofanya ziara katika kiwanda hicho.
Baadhi ya wakaguzi wa chakula cha mifugo wakimsikiliza Katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel(hayupo pichani)
****************************************
NA FARIDA SAID, MOROGORO
Katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel amewataka wafugaji kote Nchini kuacha tabia ya kufuga kizamani badala yake kufuga kitaalamu kwa kutumia chakula kilicho bora na kaguliwa na wakaguzi wa chakula cha mifugo waliopitishwa na waizara hiyo ambao wapo kila mkoa, hali itakayosaidia kupunguza magonjwa na kuongeza uzarishaji.
Katibu mkuu Ole Gabriel ameyasema hayo Mkoani Morogoro wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa wakaguzi wa chakula cha mifugo kutoka kanda ya mashariki inayounganisha Mikoa ya Dar Es Salaam,Morogoro,Tanga, Pwani na Dodoma,ambapo amewataka kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kazi na muungozo wa sharia pasipo kumuone mtu
“Msikubali kufanya kazi kwa mazoea fanyeni kazi kwa weledi na msipokee wala kutoa rushwa kwa namna yeyeyote ile ni kinyume cha maadili ya kazi”. Alisema Prof.Elisante Ole Gabriel
Aidha Katibu mkuu huyo ametoa lai kwa taasisi zote zinazo zalisha chakula cha mifugo hapa nchini kufanya tafiti za kina katika malighafi zote zinazotumika katika kuchata chakula kama zinakidhi vigezo vya kutumika kama chakula cha mifugo,huku akiwataka wakaguzi kusimamia vyakula vyote vinavyozalishwa katika viwanda kabla ya kufika kwa mtumiaji wa mwisho.
Pia amewataka wafugaji kutumia chakula kinachozalishwa katika viwanda vinavyotambulika na kusaliwa na selikari, kwani chakula kinachozalishwa mtaani kinakosa ubora unaohitaji kwa matumizi ya mifugo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uendeshaji wa malisho na vyakula vya mifugo Dk Asimwe Rwiguza ameataka wafugaji kuacha dhana potofu ya kulisha mifugo chakula ambacho hakifai kwa binaadamu na kusema kuwa chakula kisichifaa kwa binaadamu pia hakifai kwa mifugo.
Pia amewataka wakaguzi wa chakula cha mifugo waliopata mafunzo hayo kwenda kutoa elimu kwa wafugaji namna bora ya kufuga kwa kuzingatia ufugaji wa kisasa.
Hata hivyo wakaguzi wa chakula cha mifugo hao walipata fulsa ya kutembelea kiwanda kinachozalisha chakula cha mifugo cha International Tanfeeds Ltd kilichopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kujionea hali ya uzalishaji.