**********************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (MNEC),mkoani Pwani ,Haji Jumaa, amewataka wananchi mkoani Pwani kutofanya ajizi tarehe 28 ,oktoba mwaka huu kwa kucheza pata potea kuchagua wapinzani na badala yake waichague CCM kuanzia Rais,wabunge na madiwani.
Aidha ameeleza miaka mitano ya Rais Dkt. John Magufuli ameiwezesha Msajili wa Hazina ya Serikali kuokoa shilingi Tirioni 1.053.
Haji alisema ,hayo Janga ,Mlandizi mkoani Pwani na kudai CCM inastahili kushika dola kwa miaka mingine mitano kwani imefanya makubwa nchini katika miaka mitano iliyopita.
Alieleza wapinzani hawana chao kwakuwa CCM imetekeleza mengi kiuchumi na kimaendeleo hatimae kufikia uchumi wa kati .
Hata hivyo Haji anabainisha, chombo hicho kilichokuwa tangu Uhuru, kwa mara ya kwanza katika utawala wa Dkt. Magufuli umeweza kulipatia Taifa kiasi hicho cha fedha, kutoka katika mashirika na makampuni ikiwemo ya Airtel ambapo wa-Tanzania wanamiliki kwa asilimia 49.
Alisema , sanjali na kiwango hicho cha fedha, pia imeweza kuhakiki Makampuni 81, huku 54 kati ya hayo yamepeleka gawio la Serikali la shilingi tirioni 1.057, kutoka bilioni 100 zilizokuwa zinakusanywa kabla ya kuingia kwa Dkt. Magufuli.
“Hapa Mlandizi tumeletewa zaidi ya shilingi bilioni moja zilizojenga Hospitali yetu pale Kilangalanga, kwa hiyo kwa kiwango kilichookolewa na Hazina kina uwezo wa kijenga Hospitali kama zile elfu moja, hapo utamsikia mtu anasema Magufuli hajafanya kitu,” alisema Haji.
Aliongeza katika kipindi hicho pia imefanikiwa kuokoa viwanja 140 mai ya serikali sanjali na nyumba 377 zilizokuwa zinamilikiwa na viongozi mbalimbali wa mashirika na Makampuni ya uma, ambayo kwa sasa vipo chini ya Serikali.
“Hivi karibuni benki ya NMB imeipatia serikali gawio la shilingi bilioni 10, ambazo zitatumika kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo, huku akiongeza kwamba hakuna kiongozi anayeweza kufanana na Magufuli,” alisema Haji.
Alisema kuwafananisha wagombea wengine na Magufuli ni sawa na kutoitendea haki akili, kwani ni viongozi ambapo hawafanani na Magufuli, huku akiwataka wana-Janga, Kibaha Vijijini na nchi kwa ujumla Oktoba 28 kumchagua kwa kura nyingi Dkt. Magufuli na wagombea wote wa CCM.