Mkurugenzi Mstaafu Mosses Mabula akiongea kwenye kikao cha wadau wa uchaguzi kilichoandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa na chama cha wanasheria wanawake nchini Tawla jijini Arusha mapema leo
Mratibu wa semina hiyo kutoka Chama cha wanasheria wanawake nchini Tawla Happyness Mfinanga akitoa maelezo mbele ya wadau wa uchaguzi kwenye semina ya wadau hao mapema leo jijini Arusha
Wadau wa Uchaguzi wakifuatilia kwa makini mada zilizoendeshwa na muwezeshaji Firmin Miku hayupo pichani mapema leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
Picha ya pamoja.mara baada ya kumalizika kwa kikao cha wadau wa uchaguzi kilichofanyika leo jijini Arusha
……………………………………………………………………………..
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wadau wa Uchaguzi wameaswa wakati wote wa zoezi la uchaguzi kusimamia sheria kanuni na taratibu ,kuheshimu,kulinda,na kutenda haki ili mwisho wa siku kama taifa tubaki salama.
Akizungumza wakati akifungua Semina ya wadau wa uchaguzi mkoa wa Arusha iliyoandaliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa na TAWLA mapema jana Mchumi na mkurugenzi Mstaafu Moses Mabula alisema kuwa taifa linahitaji wanaopewa dhamana kutenda haki na kuhakikisha Amani inalindwa kwa nguvu zote bila kuweka tamaa.
“Niwasihi sana wasimamizi wasaidizi ngazi jimbo na kata kutenda kazi zao kwa mujibu wa sheria na kuacha mihemuko ya wanasiasa ambao mara nyingi wanakuja na matokeo mifukoni”
Alieleza kuwa watambue kuna maisha baada ya uchaguzi na taifa linahitaji viongozi wenye maono ya maendeleo ambao wananchi wameona wanawafaa kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kupita box la kura hivyo wajibu wao ni kuongozwa na sheria kanuni na taratibu zilizopo na sio vingine.
Awali Chama cha wanasheria wanawake nchini TAWLA katika kufanikisha uchaguzi mkuu wa oktoba kineendesha semina kwa wadau wa uchaguzi mbalimbali katika wilaya 5 za mkoa wa Arusha.
Aidha chama hicho kimesema kuwa lengo la semina hizo ni kuandaa wananchi kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu huo kwa Amani na utulivu na kufuata sheria na kanuni bila uvunjifu wa Amani.
Akiongea kwenye Semina hiyo ya Siku moja iliyofanyika jijini hapa mapema Jana Happyness Mfinanga alisema kuwa chama hicho lengo lake ni kuhamasisha jamii kuendeleza kutetea na.kulinda haki za mwanamke.
Alisema kuwa Chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinatoa elimu kwa umma ili kufanya uchaguzi kuwa huru na wa haki ikitambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi na pindi Amani inapotoweka wanaopata madhara makubwa ni kinamama na watoto.
“Uchaguzi huru na haki unawezekana iwapo kila mmoja wetu atafuata sheria ndio maana tumeita wadau wote wa uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha tunajadili kwa pamoja na kupata uelewa wa masuala yote ili uchaguzi upite salama”
Akizitaja wilaya zilizopata semina hiyo kuwa ni pamoja na Karatu Ngorongoro Monduli Longido na Arusha jiji
Mmoja ya wadau hao mwanachama na muanzilishi wa chama cha wanasheria wanawake nchini Mwanasheria Matilda Philip alisema sera na ilani nyingi za vyama vya siasa zimekuwa hazitekelezi sheria za mtoto kikamilifu.na.hivyo kujikuta kundi hilo likisahaulika sanjari na jinsia ikiwemo uzalilishaji.
Nae Mwezeshaji wa semina hiyo Firmin Miku alisema kuwa uchaguzi ni sehemu moja ila kila moja anaowajibu mkubwa wa kuendelea kutunza Amani na usalama wakati wote wa uchaguzi hususani vyama vya siasa kuepuka lugha zisizofaa ikiwemo uchochezi.