NA
MWANDISHI WETU
WAZIRI
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewataka Mameneja wa Shirika la Umeme nchini
TANESCO wa ngazi za Kanda, Mikoa na Wilaya kuhakikisha umeme haukatiki katika
kipindi chote cha uchaguzi mkuu hususan siku ya kupiga kura.
Dkt.Kalemani
ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2020 baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo
cha kupoza na kusambaza umeme Megawati 48 cha Dege wilayani Kigamboni jijini
Dar es Salaam.
“Maeneo
yote kuanzia kwenye vijiji, kata wilaya na mikoa nchi nzima umeme usikatike
wakati wa uchaguzi, usikatike maeneo yote na muda wote lakini hasa hasa wakati
wa kupiga kura tarehe 28, Oktoba, tunataka wananchi wapige kura kwa uhuru na
uhakika.” Alisisitiza Dkt. Kalemani ambaye alifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na viongozi wengine wa wizara.
Akizungumzia
kuhusu kituo hicho cha kupoza na kusambaza umeme cha Dege, Dkt. Kalemani
alisema ujenzi wake umefikia asilimia 81 na amewaagiza wakandarasi kuhakikisha
ifikapo Novemba 2020 ujenzi uwe umekamilika kwa asilimia 100.
Alisema
ametembelea kituo hicho mara sita na lengo ni kuhakikisha wananachi wa Kigamboni
wanapata umeme wa uhakika wakati wote.
“Niwapongeze
TANESCO na Mkandarasi kwa hatua mliyofikia ingawa Mkandarasi aliomba miezi
miwili kukamilisha kazi hii mimi nimesema hapana, kwanza kazi yenyewe iliyobaki
ni ndogo hivyo nimetoa mwezi mmoja kufikia Novemba ujenzi uwe umekamilika.”
Alisisitiza Dkt. KJalemani.
Waziri
aliwasifu wahandisi wazalendo kutoka TANESCO kwani mafundi wa kujenga kituo hiki
ni TANESCO wenyewe Mkandarasi kutoka Crotia anasimamia tu na kutoka hapa tutakuwa
tumepata ujuzi wa kutosha kuanza kujenga vituo vyetu sisi wenyewe na tayari
tumeanza kule Tabora pamoja na Katavi wanasimamia na kujenga TANESCO wenyewe.
Alisifu Dkt. Kalemani
Aliisifu
Serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya umeme
kwani katika kipindi cha miaka mitano jumla ya vituo vya kupoza na kusambaza
umeme vikubwa na vidogo 141 vimejengwa nchi nzima.
Akitoa
taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Meneja Mradi, Mhandisi Neema Mushi alisema
mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 26. 2 ikijumuisha na ulipaji
fidia kwa wakazi waliohamishwa kupisha mradi.