Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Victor Kategere akifungua kikao kazi cha ziara ya viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibari kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamuhanga leo Jijini Dodoma.
Muonekano wa Ukumbi wa kikao kazi cha ziara ya viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibari leo jijini Dodoma Baadhi ya Wataalamu wa Tehama walioshiriki kikao kazi cha ziara ya viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibari leo Jijini DodomaMkurugenzi wa Tehama TAMISEMI, Erick Kitali akitoa wasilisho la mifumo leo Jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha ziara ya viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibari
………………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim , Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Victor Kategere amesema kuwa Mifumo ya tehama imekuwa chachu ya udhibiti wa upotevu wa mapato katika kukuza uchumi wa Taifa.
Mkurugenzi Kategere amebainisha hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha ziara ya viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibari kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamuhanga .
Aidha Mkrugenzi Kategere amesema kuwa uwepo wa mifumo madhubuti katika mamla za serikali za mitaa imepelekea kuongezeka kwa mapato yanayosaidia kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.
Akiwasilisha wasilisho la Mifumo Mkurugenzi wa Tehama TAMISEMI, Erick Kitali ameeleza uwepo wa mifumo imesaidia serikali kupunguza gharama kubwa kwa watendaji watendaji wa halmashauri waliokuwa wakisafiri kuja Dodoma na kutengeneza bajeti na mipango za halmashauri zao kwani sasa zinatengenetwa kupitia mifumo na kuwasilisha taarfa wizarani.
“Ili ukusanye mapato kwa haki lazima kutoa huduma bora kwa wananchi hivyo hakuna kinachoshindikana kwenye Tehama kwani leo tunaoana watanzania walivyo rahisishiwa upatikanaji wa Huduma kupitia mifumo iliyotengenezwa na wazawa kwa kutoanza kupanga foleni katika maofisi ya umma ” ameeleza Kitali.
Lakini pia Kitali ameeleza kuwa mifumo hiyo imetengenezwa na watanzania hivyo ni rahisi kutatua changamoto pale panapo jitokeza changamoto katika mifumo hiyo na wapowataalamu kwa ajiri ya usalama wa mifumo hiyo ili kutoingiliwa na kutumiwa vibaya.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa TAMISEMI, Shomari Mukhandi ameeleza kuwa mapato ya ndani ya Halmashauri yanatokana na Mamlaka ya kisheria Sura Na. 287,288 na 290.
Vile vile Mukhandi amesema Halmashauri zimepewa mamlaka ya kukusanya kodi , ushuru, ada na tozo mbalimbali ili kutekeleza majukumu yake ya kisheria yakiwemo kutoa huduma za kijamii , kuimarisha ulinzi na kudumisha amani kwa kuinua uchumi wa wakazi wa himaya za mamlaka hizo.
“Nitoe rai kwa Viongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) kuhakikisha mnakusanya mapato kwa watu sahihi na kutenda haki katika ukusanyaji wa mapato bila kuwakandamiza wananchi”, amesisitiza Mukhandi.
Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango OR-TAMISEMI , John Cheyo, amesema TAMISEMI inafanya vema katika shughuli zake na hayo ni matokeo ya ugatuzi wa madaraka , uwajibikaji na ushirikiano mzuri uliopo katika watendaji wa ofisi hiyo.