Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Arch.Elius Mwakalinga akifungua
mkutano Mkuu wa kwanza wa mwaka Bodi ya
Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB)uliofanyika 15 oktoba
2020, katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB) Edwin
Nnunduma akielezea mpango wa kusajili kampuni na wataalam katika sekta hiyo
wakati wa mkutano Mkuu wa kwanza wa
mwaka Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB) uliofanyika 15 oktoba 2020, katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam.
Majenzi (AQRB) Arch. Dkt Ludigija Bulamile akifafanua
jambo wakati wa mkutano huo,
huo.
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elius Mwakalinga (katikati
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
watalaam wa sekta ya ujenzi wakati wa mkutano Mkuu wa kwanza wa mwaka Bodi ya Usajili wa Wabunifu
Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB uliofanyika 15 oktoba 2020, katika ukumbi
wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE
NA PHILEMON SOLOMON
SERIKALI
imesema hadi kufikia januari mwakani
itaanza kuwawajibisha kwa kuzichukulia
hatua Kampuni za ujenzi, wabunifu majengo na wakadiliaji majenzi ambao watakuwa
hawajajisajili.
Akizungumza
katika mkutano Mkuu wa kwanza wa mwaka
wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB), Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elius Mwakalinga, alisema
kuwa hadi kufikia januari 2021 wataalamu wote wa sekta ya ujenzi wanatakiwa kuwa
wamejisajili ili kuhakikisha kwamba kila anayefanya shughuli
hizo awe ni mtaalam na si kuwaachia wasio na taaaluma kufanya shughuli hizo.
“Hii ni
taaluma muhimu na nyeti kwa uchumi wa nchi yetu, tuko katika ujenzi wa uchumi
wa viwanda, na juhudi hii haiwezi kufikiwa katika malengo yake kama hakuna
wataalam wa uhakika katika sekta hii, na ndiyo maana tunataka tuhakikishe wote
wanasajiliwa na tunawatambua,”alisema Mwakalinga.
Alisema tunataka shughuli zote sifanywe na wataalam na siyo kuruhusu watu
wasio sahihi kuvamia sekta hii na kuharibu, na usajili huu utarahisisha
kuwatambua wavamizi na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Lengo ni kuongeza
udhibiti wa shughuli za wataalam wasiosajiliwa na kufanya kazi bila kuwa na
leseni.”
Mwakalinga
alisema pia kwa sasa serikali inaandaa mfumo maalum wa ufuatiliaji wa
uendeshaji wa vivuko nchi nzima kwa kufunga vifaa maalum (GPS)ambavyo
vitasaidia kurekodi uendeshaji wake.
Aliongeza
kuwa pamoja na mambo mengine mfumo huo unalenga kudhibiti uharibifu wa
miundombinu na kusaidia kupunguza ajali zisizo za lazima.
“Hatua hii
ya kufunga GPS iko kwenye mchakato na tunatarajia kwamba mpaka Januari mwakani
tutakuwa tumekamilisha.
Mfumo huu utatusaidia pia kufahamu pale kivuko
kinapozidisha mzigo au kufanya shughuli zake kinyume na taratibu, hata tukiwa
ofisini tutakuwa tunaona,”alisema Mwakalinga.
Kwa upande
wake, Msajili wa Bodi hiyo, Edwin Nnunduma, alisema mpango wa kusajili kampuni
na wataalam katika sekta hiyo utasaidia
kupunguza malalamiko mengi ambayo wamekuwa wakipokea kutoka kwa baadhi ya
wavamizi wa taaluma hiyo pale wanapoharibu kazi.
Nnunduma
alisema hadi kufikia Septemba mwaka huu, bodi hiyo ilikuwa imesajili Wataalam 1,126
na makampuni ya kitaalam 381.
“Wakati bodi
inaanza wataalam waliosajiliwa walikuwa 188 na makampuni ya kitaalam 53,
ongezeko hili ni kubwa lakini ukilinganisha na na uhitaji wa huduma za wataalam
nchini , idadi hii bado ni ndogo,”alisema Nnunduma.