SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa ratiba ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika zitakazofanyika kuanzia Januari mwakani nchini Cameroon na wenyeji, Simba Wasiofungika watafungua dimba na Zimbabwe Januari 14 Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé.