Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt Hamis Kigwangallah akizingumza wakati akifungua Mkutano Mkuu baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari Waandamizi ,Mkutano unaofanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya Washiriki katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mgeni rasmi ,Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt Hamis Kigwangallah (hayupo pichani)
Washiriki katika Mkutano huo ambao ni Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi wakiwa katika ukumbi wa Mikutano katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza .
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Dkt,Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo .
Mkutano huo unawahusisha baadhi ya viongozi waandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari waandamizi kutoka mikoa mbalimbali nchini .
Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara -TANAPA,William Mwakilema akizungumza katika Mkutano huo.
Mkurugenzi wa ABM Radio ,Abdalah Majura akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa mkutano huo mara baada ya Mgeni rasmi ,Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamis Kigwangallah kuufungua rasmi .
Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV.
WAZIRI wa Malisili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangallah amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kufungua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato siku ya Jumanne ya Julai 9/2019 .
Dkt Kigwangallah ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari nchini ,mkutano unaofanyika jijini Mwanza.
Amesema pia Serikali inakamilisha mkakati wa kuanzisha utalii wa Majini katika maeneo ya Hifadhi na Vivutio vilivyopo ndani na Pembezoni mwa Ziwa Victoria “Boti Maalumu kwa ajili ya kusafirisha watalii kati ya maeneo ya Hifadhi zilizopo katika ukanda huu inatarajia kufika Mwanza hivi karibuni “alisema Dkt Kiwangallah .
akimkaribisha Dkt Kigwangallah ,Kamishna wa Uhifadhi (TANAPA) Dkt Allan Kijazi amesema mkutano huo unafanyika kwa miaka sita mfululizo ni mkakati wa kuwawezesha wana habari kufahamu na kuelewa masuala ya Uhifadhi ili waripoti kwa usahihi mambo mblimbali yanayohusua Uhifadhi na Utalii kwa ujumla.
Mwisho