Mkuu wa wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi akihutubia wananchi, wazazi na wanafunzi wakati wa sherehe za mahafali ya kuhitimu kidato cha nne kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari.Mandewa wanaosali Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), mkoani hapa jana.
Wanafunzi, wananchi na wazazi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wananchi na wazazi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Watoto wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wake wa wachungaji wa kanisa hilo wakiwa kwenye mahafali hayo.
Askofu wa kanisa hilo, Gasper Mdimi (kushoto) Mchungaji Abeli Manupa na Mwalimu Mkwiye Emmanuel (kulia) wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mahafali yakiendelea.
Wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Mhitimu, Faraja Nyambi.
Mkuu wa wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Mhitimu, Betha Isaya.
Mkuu wa wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akimkabidhi cheti Mhitimu, Alex Stephano.
Mahafali yakiendelea.
Wahitimu hao wakiombewa.
Mgeni rasmi Mkuu wa wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi na viongozi wa kanisa hilo wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
Mkuu wa wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi na viongozi wa kanisa hilo wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kiislamu waliofika kanisani hapo kushiriki na wenzao kwenye mahafali hayo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa
Singida, Dk. Rehema Nchimbi amesema serikali haitasita kumchukulia hatua mtu
yeyote atakayehatarisha amani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.
Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo alipohutubia wananchi, wazazi na
wanafunzi wakati wa sherehe za mahafali ya kuhitimu kidato cha nne kwa Wanafunzi wa Shule
ya Sekondari ya Mandewa wanaosali Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC), mjini hapa jana.
“Kuna watu fulani fulani wanazungumza maneno yenye kila
aina ya viashiria vya uvunjifu wa amani wakidhani huenda kipindi hiki cha
kampeni serikali haipo kazini. Niwatahadharishe kamwe wasithubutu kufanya hivyo
wataishia kwenye mkono wa sheria,” alisema na kuongeza:”Mpaka mda huu
serikali ipo, na Rais wetu sote bado ni Dk. John Pombe Magufuli.
Katika hatua nyingine, ‘Mama’ Nchimbi alimpongeza Rais kwa
ujasiri,na maono yake kwa namna ya pekee alipofanikiwa kulivusha salama Taifa
dhidi ya janga hatari la Corona.
“Haya maamuzi sio mepesi mepesi tazameni nchi nyingine
zinavyoendelea kuteseka mpka sasa…kwakweli tunamshukuru sana Rais na Mwenyezi
Mungu aendelee kumuongoza na kumjalia hekima na busara ili mapenzi yake ya
dhati kwa watanzania wenzake yazidi kushamiri.”
Aidha, katika mahafali hayo yaliyofanyika kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of God la Evangelistic Christian Centre (ECC),
Nchimbi aliwakumbusha wazazi kuepuka kuwapa simu watoto wawapo masomoni ili
kuwajengea nidhamu ambayo itakuwa ni msingi wa ufaulu na mafanikio yao kwenye
tafakari ya masomo.
Akizungumzia maisha ya wahitimu hao baada ya kidato cha nne,
aliwaasa kuwa waangalifu na kuepuka mitego na vishawishi vya kidunia ambavyo
vinaweza kuwatumbukiza katika mashimo ya dhambi na kuharibikiwa, ikiwemo
kupoteza ndoto zao njema za maisha walizonazo.
Kwa upande wake, Askofu wa kanisa hilo, Gasper Mdimi aliwataka
wahitimu hao kutafakari sambamba na kuchukulia mahafali hayo na malezi
waliyopewa kwa kipindi chote kama kiapo chao kwa Mungu cha kutotenda dhambi
wala kurudia kutenda dhambi na wasisahau kila mmoja kuendelea kulinda usafi wa
moyo popote pale watakapokuwepo.