NJOMBE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na Mgombea urais kupitia CCM Dokta John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vimewakamata watuhumiwa Wote wa mauaji ya Kijana Emmanuel Mlelwa aliyekuwa Mwenyekiti wa wanafunzi wa Vyuo vikuu wa CCM mkoa wa Iringa .
Rais Magufuli ametoa agizo Hilo akiwa Mjini Makambako Wakati wa mkutano wake wa Kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 28 Mwaka huu na kwamba uchunguzi wa Kina ufanyike na wafikishwe Mahakamani.
Wakati akiomba kura kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe Dokta Magufuli amesema kiasi Cha shilingi Bilioni 498.76 Zililetwa Katika Mkoa wa Njombe kutekeleza miradi mbalimbali Ya Barabara Katika kipindi Cha miaka mitano pekee.
Awali akizungumza kabla ya Dokta Magufuli Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Mzee Philip Mangula amesema kuwa kinachotakiwa kwa wanaccm na Wananchi hapo Oktoba 28 Mwaka huu Ni kwenda kupiga Kura na kuondoka badala ya kusalia vituoni kwani kazi ya kulinda Kura sio yao.
Kwa Upande Wake Mgombea Ubunge Jimbo la Makambako Deo Sanga Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Amesema Kuwa Fedha Zilizotengwa Katika Jimbo Lake Zaidi ya Shilingi Bilioni 40 Zitakwenda Kutekeleza Miradi Mingi na Mikubwa Likiwemo Tatizo Sugu la Maji Mjini Hapo.
“Jimbo la Makambako limetengewa kiasi cha bil 40 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya maji ambayo ndiyo limekuwa tatizo kubwa la mji huu” Alisema Deo Sanga
Nae Rebecca Nsemwa mgombea Ubunge viti maalumu mkoa wa Njombe amesema watanzania wanakila sababu ya kumpa kura rais Magufuli katika uchaguzi mkuu ili aweze kkuendelea kufanya mambo mazuri ambayo ameanza kufanya kwa kipindi cha miaka 5
Katika hatua nyingine mgombea ubunge viti maalumu mkoa wa Njombe Rebecca Nsemwa akiwaomba kura wana Njombe katika uchaguzi mkuu amesema ifikapo octoba 28 anaomba kura zote zikapigwe kwa rais Magufuli a.k.a ANT-CORONA ,Kura zote kwa wabunge wa CCM pamoja na madiwani wote ili wakaweze kuendeleza kazi ya miaka mitano ya awali.
Ninaomba kura kwa rais wetu mpendwa aka ant corona , ninaomba kura za wabunge wetu wote wa mkoa wa Njombe pamoja na madiwani wetu wote ili itakapofika tar 28 CCM ikapate ushindi wa kishindo na kuongoza tena dola”Alisema Rebecca Nsemwa.