Mkurugenzi Msaidizi, Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Maji Bw. Alex Tarimo (kushoto), akimsikiliza Afisa Tarafa wa kijiji cha Karema, wilayani Tanganyika Bw. Mbonimpaye Mtiyonza Nkoronko, anayeelea kuhusu huduma ya maji katika eneo lake la kazi, ambapo huduma hiyo inatolewa kwa saa 24, katika vituo 14 vya wananchi, na baadhi waliounganishiwa katika makazi yao.
Wataalam wa sekta ya maji wakikagua mfumo unaochukua maji kutoa ziwa Tanganyika katika mrdi wa maji wa kijiji cha Karema. Sehemu ya mradi huo imekamilishwa kwa kuwatumia wataalam wa Wizara ya Maji kupitia utaratibu wa force account.
Mkurugenzi Msaidizi, Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Maji Bw. Alex Tarimo (kushoto) akijidhirisha kuhusu upatikanaji wa maji katika kijiji cha Werema, wilayani Tanganyika ambapo wananchi wanapata huduma hiyo katika vizimba 14 vya umma.
Meneja wa wilaya wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), wa wilaya ya Tanganyika Mhandisi Alkam Omari (wa pili kushoto), akieleza jitahada zinazofanyika kufikisha maji bombani katika makazi ya wananchi wilayani Tanganyika, mkoa wa Katavi. Hali ya upatikanaji maji vijijini mkoani Katavi inawafikia wananchi kwa asilimia 62 kutoka 51 ya mwaka 2018, ambapo miradi inayoendelea itakapokamilka kiwango hicho kitafika asilimia 85. Wengine ni watendaji katika sekta ya maji nchini.
…………………………………………………………………….
Huduma ya maji mkoani Katavi inazidi kuimariki baada ya miradi ya maji iliyokuwa ikitekelezwa kukamilika na wananchi kuanza kupata huduma hiyo karibu na makazi yao.
Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Katavi Mhandisi Peter Mugula amesema kuimarika huko ni matokeo ya jumla ya miradi ya maji 14 kukamilika. Ameongeza kuwa miradi 24 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na inatarajiwa kukamilika kabla ya Desemba 2020.
Mhandisi Mugula amesema hadi mwezi Agosti 2020 asilimia 62 kutoka asilimia 51 ya wakazi waishio vijijini tayari walishapata huduma ya maji, na mjini asilimia ya ilipanda hadi 75 kutoka asilimia 40 ya wananchi waliokuwa wakipata huduma ya maji. Amefafanua kuwa mabadiliko hayo yametokana na baadhi ya miradi kukamilishwa na wataalam wa sekta ya maji kwa utaratibu wa force account.
Ameainisha kuwa miradi ya maji ya mjini inasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (MUWASA), ambapo hivi sasa mamlaka hiyo imeanza maandalizi ya kujenga mradi wa maji wa Kanoge II utakaozalisha maji mita mita za ujazo 1,200. Mradi wa Kanoge utaimarisha zaidi upatikanaji wa maji hadi kufikia mita za ujazo 8,700 hivyo kufanya kiwango cha upatikanaji maji kufika asilimia 87.
Mhandisi Mugula amesema kuwa lengo ni kuwafikia wananchi wote katika huduma ya maji na hakuna atakayeachwa. Takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa mkoa wa Katavi una jumla ya watu 564, 604 na mwaka 2018 mkoa huo ulikadiriwa kuwa na idadi ya watu 738, 237.