Ndg. Hamimu Mahamudu katibu wa siasa itikadi na uenezi Chama Cha Mapinduzi Mkoani Kagera akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba.
*******************************
Na Allawi Kaboyo Bukoa.
Mjumbea wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi na Waziri mkuu wa Jamhuri way Muungano wa Tanzania Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya kukiombea kura chama chake mkoani Kagera ambapo atafanya mikutano mbalimbali ya hadhara.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba,katibu mwenezi wa chama hicho mkoani Kagera Ndg. Hamimu Mahamudu amesema kuwa chama chao kinaendelea na kampeini za kuomba kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ujao hivyo kiongozi huyo ataanza kampeini zake za kuwaomba wananchi kukichagua kwa kuana na wilaya ya Bukoba.
“Kama tunavyojua ndg wanahabari Waziri mkuu ni mlezi wa mkoa wetu kichama hivyo kesho ataanza kampeni kama ilivyo ada atafanya mikutano akianzia Rubale halmashauri ya wiaya Bukoba na baadae jioni atakuwa na mkutano mwingine wa hadhara uwanja wa mayunga Manispaa ya Bukoba.” Amesema Hamimu.
Hamimu ameongeza kuwa Mhe.Majaliwa atakuwa na ratiba ya siku tatu katikamkoa huo ambapo atakwenda pia Kyerwa,Missenyi Karagwe Ngara na baadae kumalizia Biharamulo wakati akielekea mkoani Geita abapo amewaomba wananchi kujitokeza hasa katika maeneo ya mikutano.
Aidha amewaomba wananchi wa mkoa wa Kagera kuwa nje ya mikutano ya hadhara waziri mkuu atafanya mikutano ya njiani ya kuomba kura katika maeneo mbaimbali hivyo wananchi watakao kuwa katika maeneo ya njiani ambapo atapita wajitokeze kuja kumsikiliza.
Waziri Mkuu akiwa Kagera atafanya mkutano Issingilo kwa upande wa Kyerwa, Bunazi uwanja wa mashujaa kwa wilaya ya Missenyi, Kayanga Karagwe uwanja wa Changalawe na mjini Ngara pamoja na Nyakanazi kwa wilaya ya Biharamulo.