Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe(Katikati) akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Tanzania
bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaosimamia Sekta za
Utalii,Habari,Utamaduni,Sanaa, Michezo na Mambo ya Kale kilichofanyika Julai
02,2019 Jijini Dodoma. Kushoto ni Mhe.Balozi Ally Abeid Karume na Waziri wa
Habari,Utalii na Mambo ya Kale na kulia ni Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale
Mhe.Mahmoud Thabit Kombo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe,
Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Ally Abeid Karume na
Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo (Kutoka
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) wakisaini Taarifa ya Ushirikiano baina ya Serikali ya
Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Sekta wanazosimamia leo Julai
02,2019 Jijini Dodoma.Wanaoshuhudia ni Viongozi waandamizi wa wa Jamhuri ya
Muungano katika Sekta hizo.
3.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nicholas
William akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Tanzania bara na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaosimamia Sekta za Habari, Utalii
Utamaduni,Sanaa, Michezo na Mambo ya Kale kilicholenga kuimarisha ushirikiano
katika sekta hizo kilichofanyika Julai 02,2019 Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe
(kushoto) akizungumza na Wanafunzi na wanamichezo wa shule ya Foutain Gate
Academy iliyopo Jijini Dodoma ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kukuza vipaji
mbalimbali vya michezo wakati akiwatambulisha Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Balozi Ally,Abeid Karume (kulia) na Waziri wa Habari,Utalii na
Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kulia) kutoka Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar walipoitembelea shule hiyo leo Julai 02,2019.
Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo kutoka
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akifurahia zawadi ya sabuni aliyopewa na Uongozi wa
wa Shule ya Foutain Gate Academy mara baada ya kuitembelea shule hiyo iliyopo
Jijini Dodoma leo Julai 02,2019. (PICHA NA SHAMIMU NYAKI- WHUSM).
*************
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja
na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo
na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume
wamesaini makubaliano ya ushirikiano katika kusimamia na kutekeleza sekta za Habari, Utamaduni,Sanaa na michezo ili kuongeza tija.
Uwekaji wa saini za ushirikiano huo umefanyika leo Jijini Dodoma katika ukumbi
wa chuo cha Ufundi Veta, baada ya vikao vya ngazi za wataalam na Makatibu
Wakuu wa Wizara husika kuwasilisha taarifa hizo kwa Mawaziri na hatimaye kuridhia tayari kwa ajili ya utekelezaji.
“Hatua hii ni nzuri na muhimu kwetu katika kuhakikisha tunadumisha na kuhifadhi
muungano wa kihistoria ambao ulioasisiwa na waasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius
Kamabarage Nyerere na Shehe Amani Abed Karume” Alisisitiza Dkt. Mwakyembe.
Aidha, Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit
Kombo ameeleza kuwa katika sekta ya habari ni muhimu kwa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) kushirikiana na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ili kuandaa vipindi mbalimbali ikiwemo kipindi cha utalii Safari chaneli.
“Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya utalii nchini , vyombo hivi vya habari TBC
na ZBC vinapaswa kushirikiana kuandaa vipindi vya utalii ili kuitangaza sekta hii
nje na ndani ya nchi” Alisisitiza Mhe. Mahmoud Thabit Kombo .
Kwa upande wake Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally
Abeid Karume amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili
inatangazwa na kuenezwa kuna umuhimu wa kuandaa kanzi data itakayojumuisha
wataalam wa Kiswahili ambao watakuwa wakifundisha wageni ndani na nje ya nchi.
“Tanzania imechangia sana katika kukuza lugha ya Kiswahili na watu wengi
wanapenda kuja kujifunza kwetu ,hivyo naamini kwa kuwa na kanzi data hii
itasaidia sana katika kuwapata watalaam wazuri wa kufundisha lugha hii”. Balozi Ally Abeid Karume.
Vilevile Mawaziri hao wamekubaliana kuimarisha ushirikano katika sekya ya sanaa
kwa kuhakikisha kuwa ifikapo desemba 2019 wanakuwa wamesha andaa kanuni
zitakazowawezesha watayarisha wa filamu kutoka nje ya nchi ili kuruhusu
utumiaji wa maudhui hayo kwa vyombo vya habari vya serikali.