Mtafiti kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa shamba, kulipima na upandaji wa zao la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma jana katika shamba la Magereza la wilaya hiyo.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Lufu, Pascal Male (kushoto) na wenzake wakijifunza kutoka TARI namna ya kuweka alama wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho kabla ya kupandwa zao hilo.
Maafisa Ugani na Wakulima wakijifunza kwa vitendo namna ya upimaji wa shamba la korosho kabla ya kupanda.
Mkulima kutoka Kata ya Lupeta, Yohana Mkasanga (Aliye chuchumaa akipima shamba kwa kamba katika mafunzo hayo ya vitendo. Kushoto (mwenye kofia) ni Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, Dkt.Geradina Mzena akiwa kwenye mafunzo hayo.
Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Mpwapwa, Kongwa, Malizia Said (kulia), akijifunza kutoka TARI namna ya kuweka alama wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Ving’hawe, Bhoke Magere (kulia) na wenzake wakijifunza kutoka TARI namna ya kuweka alama wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Maafisa kilimo wakijadiliana jambo kwenye mafunzo hayo kwa vitendo. Kutoka kushoto ni Afisa Kilimo kutoka Kata ya Chuyu, Oscar Masamalo, Elirehema Elinisafi kutoka Kata ya Pwagi na Monica Malika kutoka Kata ya Ving’hawe.
Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, Dkt.Geradina Mzena (katikati) akielekeza namna ya upimaji wa shamba kwenye mafunzo hayo.
Mtafiti kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya kulipima ukubwa wa shimo kabla ya kuchimbwa na upandaji wa zao la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwawa.
Mkulima Mary Mahinyila kutoka Mpwapwa mjini, akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba hilo la Magereza la wilaya hiyo.
Mkulima Joseph Kodi kutoka Kata ya Mazai, Kijiji cha Kisokwe, akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba hilo la Magereza la wilaya hiyo.
Mtafiti kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya upandaji wa zao la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwawa.
Maafisa Kilimo na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakiangalia mkorosho ambao upo kama kichaka kwa sababu ya kuto pogolewa na kuhufanya husistawi vizuri.
Mtafiti wa Kilimo kutoka Tari Naliendele, Selemani Libaburu, akitoa mafunzo ya jinsi ya kupogolea mkorosho huo ambao umekuwa kama kichaka.
Muonekano wa mkorosho huo baada ya kupogolewa.