MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia
(NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira akisikiliza mawazo ya wenyeviti wa serikali za mitaa |
(NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira akisisitiza jambo kwa wenyeviti wa serikali za mitaa
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia
(NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira akisikiliza maoni ya wenyeviti wa serikali za mitaa
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia
(NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira kushoto akichukua mawazo ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa kata ya Nshambya |
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa wa Kata ya Kahororo |
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia
(NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira ameteuliwa kuwa mlezi wa Chama
cha Mapinduzi kata za Kahororo na Nshambya wilaya ya Bukoba mjini.
Uteuzi huo umefanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bukoba Mjini
na leo Septemba 26 mwaka huu baada ya kupokea barua ya kutaarifiwa juu
ya majukumu hayo, tayari mlezi huyo amekwisha kuanza kampeni za
kisayansi kata hizo mbili zilizopo kwenye Jimbo la Bukoba mjini.
kwa kutambua ukaribu wao na jamii, aliona ni vyema kabla ya kupanga
mikakati ya kisayansi akutane na wenyekiti wa serikali za mitaa yote
kwenye kata hizo mbili.
Alisema lengo la kukutana nao ni kupata tathimini ya hali halisi kwa
mtizamo wao na kupata uelewa wa maeneo gani ambayo kwa kushirikiana
wanaweza kuweka mikakati ya kisayansi .
“Lakini pia kuwasilisha kwao mawazo yangu ya awali ili niweza kupata
maoni yao na sasa baada ya kukutana nao kwa nafasi yao yenye umuhimu
mkubwa sana nitakutana na viongozi wenzangu CCM na Jumuiya za UWT, UVCCM
na Wazazi ngazi za Wilaya, Kata na Matawi kwa lengo la kuweka mikakati
ya Kisayansi ambayo nitairatibu” Alisema.
Aidha alisema kwamba jitihada hizo zinaenda sanjari na jitihada zingine
ambapo kwa ujumla watahakikisha Chama Cha Mapinduzi kinapata ushindi wa
kishindo kwa upande wa Urais, Wabunge na Madiwani kwenye uchaguzi mkuu
ujao.
“Kwa upande wa Jimbo la Bukoba Mjini nimepangiwa pia mitaa miwili ya
Kata za Kashai huku Kata ya Kahororo ikiwa na mitaa mitano na kata ya
Nshambya ikiwa na mitaa mitatu” Alisema
Hata hivyo alisema kwamba katika kipindi cha kampeni sambamba na
kukutana na makundi ya NGOs mbalimbali ataendesha kampeni za kisayansi
katika mitaa 10 aliyopangiwa kati ya 66 ndani ya Jimbo la Bukoba Mjini.