Khalfan Said
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamewasogezea karibu huduma Wanachama wa Mifuko hiyo katika msimu huu wa Maonesho ya 43 ya Bishara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba.
Wakizungumza leo Julai 2, 2019 kwa nyakati tofauti Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo, Bw. Hoseah E. Kashimba
(PSSSF) na Bw. William Erio (NSSF) wamesema kuwa wameamua kufanya maonesho hayo kwa kushirikiana ili kuwarahisishia Wanachama kupata huduma wanazohitaji wote wakiwa kwenye banda namba 13 lililo mkabala na jingo la matangazo ndani ya viwanja vya Sabasaba.

“Tukiwa katika banda hili kwa kushirikiana na wenzetu wa NSSF ambao wao wanashughulika
na wafanyakazi kutoka Sekta Binafsi na sisi PSSSF tunahudumia wafanyakazi
kutoka Sekta ya Umma.”
na wafanyakazi kutoka Sekta Binafsi na sisi PSSSF tunahudumia wafanyakazi
kutoka Sekta ya Umma.”
Tumeona
tufanye maonesho haya pamoja kwa sababu ya kutoa elimu kwa wanachama kwa urahisi zaidi hasa kwa vile hatuko katika ushindani kama ilivyokuwa hapo awali, hii itasaidia kama Mwanachama anataka kujua taarifa kuhusu Mafao yake kama anatoka Sekta binafsi ataelekezwa aende NSSF na kama anatoka Sekta ya Umma ataelekezwa aende PSSSF, amefafanua Bw. Kashimba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. William Erio alisema “Baada ya kuunganishwa Mifuko hapo mwaka jana bado watu hawajaelewa vema tofauti zilizopo kwa hiyo wanakuja hapa kama banda pekee linalotoa huduma ya Hifadhi ya Jamii na wakifika basi wanaelekezwa katika sehemu husika na kupata huduma wanayohitaji.”
Alisisitiza Bw. Erio.
Alisisitiza Bw. Erio.
Alisema ni sehemu ambayo watu wanaweza kuja na kujibiwa maswali yote waliyonayo na kutatuliwa kero zao.
Maonesho hayo ya kila mwaka yamefunhguliwa rasmi leo Julai 2, 2019 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na yanatarajiwa
kufikia kilele Jlai 13, 2019.
kufikia kilele Jlai 13, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Hoseah E. Kashimba (wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio (wapili kushoto) wakiwa na Mameneja Kiongozi Uhusiano na Elimu Kwa Umma, Bi. Eunice Chiume (kushoto) ambaye yuko PSSSF na Bi. Lulu Mengele (kulia) ambaye yuko NSSF.
Bw. Erio (kushoto) na Bw. Kashimba wakibadilishana mawazo ndani ya banda hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hoseah E. Kashimba, (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo na ule wa NSSF.