Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani akizungumza na wananchi Kitongoji cha Migombani,kijiji cha Bukene, Wilaya ya Nzega, Mkoani wa Tabora(hayapo pichani), wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme kwa kila kitongoji nchini uliofanyika, Septemba 24,2020,mkaoni humo.
Wananchi wa Kitongoji cha Migombani,Kijiji cha Bukene, Wilaya ya Nzega, Mkoani wa Tabora, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani,(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme kwa kila kitongoji nchini uliofanyika, Septemba 24,2020,mkaoni humo.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani(mwenye shati la bluu) akikata utepe kuashiria kwa uzinduzi wa usambazaji umeme katika kila kitongoji nchini uliofanyika katika kitongoji cha migombani,kijiji cha Bukene, wilaya ya Nzega, Mkoani wa Tabora,Septemba 24,2020,(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt.Philemon Sengati(kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati vijiji(REA) Wakili Julius Kalolo.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani akiweka jiwe la msingi la usambazaji umeme katika kila kitongoji nchini, uliofanyika katika Kitongoji cha Migombani, Kijiji cha Bukene, Wilaya ya Nzega, Mkoani wa Tabora, Septemba 24,2020.
Picha ya jiwe la msingi wa mradi wa usambazaji umeme kwa kila kitongoji nchini uliofanyika uliofanyika katika Kitongoji cha Migombani, Kijiji cha Bukene, Wilaya ya Nzega, Mkoani wa Tabora, Septemba 24,2020.
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma, akiwasalimia wananchi wa Kitongaji cha Ufuruma, Kijiji cha Ufuruma,Wilaya ya Uyui,Mkoani Tabora, kwenye uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme kwa kila kitongoji nchini uliofanyika Septemba 24,2020.(kulia) Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Raphael Nombo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(mwenye shati la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali ya Mkoa wa Tabora, pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Nishati,kwenye uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme wa kila kitongoji nchini uliofanyika katika Kitongaji cha Ufuruma, Kijiji cha Ufutuma,Wilaya ya Uyui,Mkoani Tabora, Septemba 24,2020.
Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati Pamoja na wafanyakazi wa Wizara na Taasisi zake, wakicheza kwa furaha mara baada ya uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa Umeme katika kila kitongoji nchini,uliofanyika katika Kitongaji cha Ufuruma,Kijiji cha Ufuruma,Wilaya ya Uyui,Mkoani Tabora.
…………………………………………………………
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Merdad Kalemani amezindua Mradi wa Ujazilizi Fungu la Pili (Densification 2 A) unaolenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vitongoji ambavyo havina umeme katika vijiji vilivyofikiwa na miundombinu.
Akizindua Mradi huo katika kitongoji cha Ufuluma Wilaya ya Uyui na Migombani Wilaya ya Nzega Septemba 24, 2020 Dkt. Kalemani alisema vitongoji ambavyo havina umeme vitaanza kusambaziwa umeme sasa. “Mpango halisi wa kuanza kupeleka umeme kwenye vitongoji unaanza rasmi leo hapa katika kitongoji cha Ufuluma mkoani Tabora” alisema.
Alisema jumla ya vitongoji 1,103 na wateja wa awali 69,079 wataunganishiwa umeme kwa kipindi cha miezi ya tisa ya utekelezaji wa Mradi huo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Philemon Sengati alitoa wito kwa wananchi kutumia vizuri fursa ya upatikanaji wa huduma ya umeme ili kufanikisha malengo ya Serikali kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo aliwahimiza wananchi kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya kuongeza kipato kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ili kubadili mfumo duni wa maisha ya vijijini.
Mradi huu unafadhiliwa na Serikali za Tanzania, Norway na Sweden pamoja na Umoja wa Ulaya kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini (REF) na utagharimu Shilingi Bilioni 142. Utatekelezwa katika mikoa tisa (9) ya Dodoma, Kilimanjaro, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Singida, Pwani, Tanga na Mbeya.