***************************************
Na Rahel Nyabali, Kigoma.
Wahitimu wa mafunzo ya mjibu wa sheria operasheni uchumi wa kati kikosi cha 824 KJ Kanembwa JKT iliyoko wilayani Kankonko Mkoani Kigoma wametakiwa kutumia vyema mafunzo waliyopata kwa manufaa ya maendeleo ya jamii ili kuweza kukuza kipato chao na jamii kwa ujumla
Yameelezwa hayo na mgeni rasimi Kanal Hosea Ndagala mkuu wa wilaya ya Kakonko iliyoko mkoani Kigoma na kuwataka wahitimu hao kutotumia mafunazo hayo kwenda kinyume cha sheria na hatua kali zitachukulia kwa mtu atakaye bainika.
Kanali Ndagala amesema kwasasa serikali ipo katika kipindi cha uchaguzi hivyo kila mtu anawajibu kusikiliza sera mbalimbali za viongozi na kumchagua kiongozi anaye mtaka.
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa jeshi la kujenga taifa nchini meja genelali chales mbuge ,Kanali Georige Kazaula amewasisitiza wahitimu hao kuwa mabarozi katika jamii kwa kudumisha uzarendo kwa kudumisha amani katika jamii kwani ndiyo chachu ya maendeleo.
Nao baadhi ya wahitimu akiwemo prospa kapima na Maria Benard wameahidi kutumia weledi walioupata katika kambi hiyo na kuwa mfano bora katika jamii.