Wakazi wa kata ya Iwungilo halmashauri ya mji wa Njombe wamesema ifikapo octoba 28 watamchagua kiongozi atakaepigania haki ya wananchi katika mgodi wa dhahabu, Shaba na Chuma ambao umegunduliwa siku za karibuni katika kijiji cha Uliwa.
Mbali na madini wakazi hao wamesema wanamtaka kiongozi atakaeweza kuinua sekta ya kilimo cha chai,viazi na parachichi ambacho mahitaji yake yanazidi kukua kila uchwao.
Wakizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya mgombea udiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo kata ya Iwungilo Regnard Danda wamesema kwa kipindi kirefu kijiji hicho kimekuwa na mgogoro na muwekezaji wa mgodi huo na kudai kwamba wanakwenda kumchagua kiogozi bila kuangalia itikadi za vyama
Mektidis Mapile na Aziz Mgala ni baadhi ya wakazi wa kijiji cha Uliwa wanasema wanataka kiongozi msomi mwenye uwezo wa kuhoji mambo ya msingi kwa watawala kwa maslahi ya Wana Iwungilo na Taifa kwa ujumla huku mgombea anaetetea kiti chake Regnard Danda akipewa chepuo kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kumaliza tatizo la barabara,afya na umeme.
Awali Sigrada Mligo mgombea ubunge wa viti maalumu kupitia chadema anasema wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya viongozi bila kujali chama ili kurejesha haki amani na maendeleo ya watu na taifa la Tanzania
Mligo ambaye ni wakili msomi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mkoa wa Njombe amesema wananchi wasione kuachana na uchaguzi wa mazoea ambao umekuwa ukiwapa wakati mgumu tangu uhuru na kwamba endapo wananchi watakipa dhamana chama chake katika ngazi zote za Urais ,Ubunge na Udiwani watakwenda kuleta mabadiliko makubwa katika taifa hili lenye utajiri mkubwa asilia.
“Tupeni dhamana ,tuchagueni ili twende ikuru ,tukamate halmashauri na tukawe na wabunge wengi ili tubadilishe katiba itakayokuwa na maslahi na nchi.Alisema Sigrada Mligo.
Kwa Upande wake mgombea udiwani ambaye anatetea nafasi yake katika kata ya Iwungilo Regnard Danda anasema endapo wananchi wata muamini na kumpa miaka mingine mitano atahakikisha anapigania mkataba wa madini ya Uliwa ukawe na maslahi kwa wananchi pamoja na kushughulikia maslahi ya uwekezaji wa kilimo cha chai na parachichi ambao umefanyika kwa kiasi kikubwa katika kata hiyo.
Aidha Danda amesema awamu iliyopita alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kufungua barabara ziendazo maeneo ya uzalishaji ,Kuanzisha mashamba ya chai na parachichi kwa kila kijiji ili kuinua uchumi wao.
“Ndugu zangu naomba mnipe kura ifikapo octoba 28 kwasababu nina kiu ya kuwatumikia na nina tosha kulingana na mambo mengi niliowafanyia.Alisema Regnard Danda.
Wakazi joto la uchaguzi likizidi kukua katika kata ya Iwungilo nako katika kata ya Njombe mjini wagombea kutoka vyama tofauti wameendelea kunadi sera zao ambapo Romanus Mayemba mgombea udiwani kata ya Njombe mjini anasema akipita atahakikisha anapambania miundombinu ya barabara zinazounganisha mitaa pamoja na maji ambayo yanapatikana na mgao licha ya Njombe kuwa na mito mingi.
“Ninaomba wanichagua ili nikawasemee halmashauri kuhusu changamoto kubwa ya barabara za mitaani ambazo ni mbovu na hili suala la maji ambali limekuwa sugu Njombe mjini.Alisema Mayemba
Katika hatua nyingine Filoteus Mligo mgombea udiwani kata ya Lugenge ambaye amepita bila kupingwa anasema punde baada ya kuapishwa atahakikisha anakwenda sera zake kuu ni afya, elimu barabara na kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo katika kata yake.
Nae Erasto Mpete mgombea udiwani kata ya Utalingolo anasema amelazimika kugombea udiwani katika kata hiyo yenye changamoto katika sekta ya miundombinu na uchukuzi,Elimu ,afya,Kilimo na umeme na kwamba mapema baada ya kupita atakwenda kusimamia na kutekeleza mambo hayo.