Kaimu Mtendaji Mkuu (TBA), Bw.Said Mndeme akiongea na Wanahabari leo katika ofisi za TBA jijini Dar es Salaam
*********
NA EMMANUEL MBATILO
Wakala wa majengo Tanzania(TBA) limewataka wapangaji wao wote wa nyumba za kuishi, biashara pamoja na wale waliopanga kwenye maeneo yao ambao wana madeni ya kodi ya pango yanayotokana na malimbikizo kulipa madeni hayondani ya Siku kumi na nne (14).
Ameyasema hayo leo Kaimu Mtendaji Mkuu (TBA), Bw.Said Mndeme katika ofisi ya Wakala wa Majengo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam, Bw.Mndeme amesema kuwa wadaiwa ambao hawatalipa madeni hayo ndani ya muda uliotolewa wataondolewa kwenye nyumba za wakala au maeneo waliopangishwa pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa mikataba walioingia na TBA.
“Wadaiwa wanatakiwa kuhakikisha wanalipa madeni yote katika muda uliotolewa. Notisi za kulipa madeni ya kodi ya pango zilishatolewa na kupelekwa kwa wadaiwa wote”. Amesema Bw.Mndeme.
Aidha, Bw.Mndeme amesema kuwa wamekuwa na jukumu la kuwapangisha watumishi wa Umma wenye sifa nyumba za kuishi za serikali pindi zinapopatikana.
Bw.Mndeme ametoa wito kwa watumishi wa Umma waliohamishwa vituo vya kazi wakiwa na madeni kulipa madeni hayo ndani ya muda uliotolewa.