Waziri kuu mstaafu Mizengo Pinda akimkabidhi mgombea Ubunge Jimbo la Arumeru mashariki ilani ya chama Cha mapinduzi wakati alipoenda kuzindua kampeni katika Jimbo hilo pamoja na kumuombea Kura Rais juzi katika viwanja vya Olbalbali vilivyopo katika kata ya Kiranyi wilaya ya Arumeru mkoani Arusha ambapo Aliwataka wananchi kutofanya kosa Tena
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Steven akimuombea Kura mgombea Urais katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za jimbo la Arumeru magharibi Juzi katika uwanja wa Olbalbali uliopo katika Kata ya Kiranyi Wilayani Arumeru mkoani Arusha
Mgombea ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi Noah Lembrus Seputu akiomba Kura katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni.
Picha na Woinde Shizza , ARUSHA)
………………………………………………………………………………..
Na Woinde Shizza , Arusha
Waziri mstaafu Mzengo Pinda amewataka wananchi wa jimbo la Arumeru Magharibi kutofanya kosa tena la kuchagua viongozi wa upinzani katika kipindi hichi cha uchaguzi bali wachague mgombea wa CCM kwani ni kiongozi ambaye ataweza kuwaletea maendeleo katika jimbo lao.
Alisema hayo juzi alipokuwa akimuombea kura Rais Magufuli pamoja na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha mapinduzi Noah Lembrusi Seputu katika uzinduzi wa kampeni ya jimbo hilo uliofanyika katika kiwanja cha Olbalbali uliopo ndani ya kata ya Kiranyi ,halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru
Pinda alisema jimbo la Arumeru Magharibi kwa muda mrefu limekosa mwakilishi sahihi wa kuwasaidia wananchi hivyo aliwataka wananchi wa Arumeru Magharibi kumchagua Noah Lembrusi Seputu ili akawasemee Bungeni na jimbo hilo liweze kunufaika zaidi na miradi ya Maendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Steven alisema kuwa japo wananchi wa jimbo hilo walifanya kaso katika uchaguzi uliopita lakini kwa kipindi hichi hawatafanya kosa tena kwani ni lazima wakamchague mgombea wa CCM kwakuwa pia wameona kazi kubwa ambazo zimefanywa na mwenyekiti wa CCM taifa .
“wanasema kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa hivyo naimani kuwa safari hii wananchi wa jimbo hili hawata rudia kosa bali watampa kura rais magufuli pamoja na mbunge na madiwani tena kura za kutosha sio za mchezo nanapenda nikuwambie mh waziri mkuu tutampa kura za kishindo Rais na tutachagua mafiga matatu”
Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo Noah Lembrusi Seputu aliwahaidi wananchi wa jimbo kuwaletea maendeleo ikiwemo kuwatengene wananchi barabara ikiwemo ya TPRI-Likamba ,Sanawari -Likamba pamoja na kutatua changamoto ya mda mrefu inaohusiana na mita 200.
Jimbo la Arumeru kwa miaka mitano iliyoisha lilikuwa likiongozwa na mbunge kutoka Chama Cha demokrasia na Maendeleo Chadema Gibson Meiseyeki ambaye kwa Mara nyingine na yeye amepitishwa na Chadema kuwania nafasi hiyo.