*******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Simba imefanikiwa kumalizia hasira zao kwa timu ya Biashara Fc baada ya kufanikiwa kuwabamiza mabao 4-0 kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Simba imepata matokeo hayo baada ya mechi ya nyuma kulazimishwa sale ya 1-1 na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
Magoli ya Simba yamefungwa na Clautos Chama Dakika 10,27 hadi mapumziko Simba ilikuwa inaongoza mabao 2-0. Kipindi cha pili Simba walizidi kuwasha moto baada ya kupata mabao mengine mawili kupitia kwa Meddie Kagere dakika 52 na goli la nne likifungwa na Mshambuliaji wao mpya Chris Mgalu dakika 85.