Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Mawakala wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Kilimanjaro ,mafunzo yaliyofanyika katika mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB mkoa wa wa Kilimanjaro walioshiriki katika mafunzo ya siku Moja yaliyofanyika katika Hoteli ya Africn Flower iliyopo mji Mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro
Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa akizungumza wakati wa mafunzo kwa Mawakala wa Benki hiyo yaliyofuguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira (kulia kwake) wengine katika picha ni Donat Mushi (kushoto) Meneja Mwandamizi wa CRDB Wakala na kulia ni Goodluck Ruhago ,Meneja Ufanisi wa Wakala kutoka CRDB Makao Makuu
Baadhi ya Mawakala wakifuatilia kwa karibu mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na maafisa kutoka CRDB Makao Makuu na Kanda ya Kaskazini
Meneja Mwandamizi -CRDB WAKALA ,Donat Mushi akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo juu ya masuala ya usalama wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kama mawakala wa CRDB
Meneja Ufanisi wa Wakala kutoka CRDB Makao Makuu ,Goodluck Ruhago akiwaeleza jambo washiriki wa mafunzo hayo yaliyohusisha Mawakala kutoka maeneo mablimbali ya mkoa wa Kilimanjaro .
Baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB mkoa wa Kilimanjaro
Meneja Mawakala Kanda ya Kaskazini ,Judica Kweka akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Baadhi ya Mawakala wa CRDB walioshiriki katika mafunzo hayo
Baadhi ya Mawakala wa CRDB mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira na viongozi wa CRDB Kanda ya Kaskazini muda mfupi baada ya kufungua mafunzo kwa Mawakala hao.
wa Benki ya CRDB katika mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo wanaofanya shughuli zao
katika mpaka wan chi jirani ya Kenya wamepewa mafunzo juu ya tahadhari na
kujiepusha na matukio ya utakatishaji fedha .
Mafunzo hayo
yaliyotolewa na maofisa kutoka CRDB Makao makuu na Kanda ya Kaskazini
yametolewa kwa mawakala kutoka maeneo ya Mwanga ,Himo ,Marangu ,Rommbo
Mkuu,Tarakea na Holili ikiwa ni muendelezo wa mafunzo yanayofanyika nchi nzima
.
Akifungua mafunzo hayo
katika Hoteli ya African Flower iliyopo mji mdogo wa Himo ,Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira alisema ni rahisi kwa wahalifu kujaribu kuwatumia
.
“Kupitia mafunzo haya
mazuri mtaweza kupewa elimu ya kumtambua mteja wako na kumuhudumia ipasavyo na
kukuwezesha kulinda na kukuza mtaji wako uweze kufanya kazi vyema zaidi.” Alisema
Dkt Mghwira .
Alisema uwakala wa
Kibenki umefungua Fursa nyingi na kuwezesha kukua kwa uchumi na kwamba serikali
inajivunia uwepo wa mawakala kwa kufungua milango ya urahisi wa kukusanya kodi
kwa kuwezesha wananchi kulipia kodi popote alipo kwa Wakala wa CRDB.
“Wakala wa CRDB ni
moja ya njia zinazoongoza kupendwa na wananchi kulipia kodi ambapo naambiwa zaidi
ya miamala millioni 8 yenye thamani zaidi ya Bil 300 zilikusanywa kupitia wakala
wa CRDB kwa Mwaka Jana tu.”alisema Dkt Mghwira
“Na kwa nusu ya mwaka
huu tayari mmesaidia serikali kukusanya
zaidi ya Bil 350..hii ni kidhihirisho kwamba uwakala wa CRDB ni
kichocheo kikubwa cha maendeleo ya Taifa kwa ujumla.”aliongeza Dkt Mghwira .
Naye Meneja wa CRDB
kanda ya Kaskazini ,Chiku Issa alisema CRDB
ndio benki ya kwanza kuanzisha huduma za mawakala wa benki ambazo ilianzisha mwaka
2013 na kwamba kwa sasa ina mawakala zaidi ya 16,000 waliotapakaa Tanzania
nzima.
“Moja ya lengo la
kuandaa semina hii ilikuwa kuwashukuru
mawakala hao katika kutambua mchango wao katika kukubali kushirikiana na benki
ya CRDB katika kupeleka huduma karibu na wateja lakini pia kuwajumuisha
wananchi kwenye huduma za kifedha (financial inclusion)”alisema Chiku
Alisema mawakala
wa CRDB wamesaidia kuongeza huduma za
kibenki kwa kuongeza muda wa wateja kufanya miamala ambapo baadhi ya mawakala
wanatoa huduma kwa masaa 24.
“Mafunzo haya yamelenga
pia kuwakumbusha mawakala kufuata taratibu na kanuni zote za kifedha kama
zinavyosimamiwa na benki kuu. Lakini pia wamepewa elimu kuhusiana na elimu ya
utakatishaji Fedha.”alisema Chiku.
CRDB imetoa elimu ya
ujasiliamali na njia nzuri zaidi ya kuhudumia wateja wa benki, pamoja na
kusaidia kuongeza wateja ili wananchi waendelee kufurahia huduma zetu lakini
pia na mawakala waweze kujipatia kipato zaidi.