Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt.Bedan Masuruli,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa onyo kwa wamiliki wa vituo vya kutolea huduma ya afya ya wanyama kuacha kuwatumia watu wasio na sifa za kutoa huduma hiyo.
………………………………………………………………………………..
Na.Rasul Kidindi,Dodoma
Baraza la veterinari Tanzania ambalo linasimamia taaluma ya veterinary na huduma za afya ya wanyama limewaonya baadhi ya wamiliki wa vituo vya kutolea huduma ya afya ya wanyama kuacha kutumia watu wasio na sifa za kutoa huduma hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt.Bedan Masuruli,wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kuwa baraza limefanya utafiti wa huduma ya afya ya wanyama katika mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Dodoma,Mara na Mwanza na kubaini kuna udanganyifu unaoendelea kufanywa na baadhi ya wamiliki wa vituo vya kutolea huduma za afya ya wanyama kwa kuwatumia watu wasio na sifa katika kutoa huduma ya afya ya wanyama na kuwasababishia wafugaji hasara.
“Wamiliki wa vituo vya kutolea huduma ya afya ya wanyma kuacha kuwatumia watu wasio na sifa katika kutoa huduma hizo wanatoa huduma zisizo na waledi na chini ya kiwango “amesema Dkt.Masuruli
Aidh Dkt.Masuruli amevitaka vituo vyote vya afya ya wanyama vyenye sifa viakikishe vinasajiliwa na vihuishe taarifa zake kabla septemba 30 kwani kati ya vituo 200 vituo vilivyo sajiliwa ni asilimia 60% na asilimia 40% bado havijasajiliwa kisheria kutoa huduma ya afya ya wanyama.
“Nasisitiza vituo vinavyotoa huduma ya afya ya wanyama kusajiliwa na kukaguliwa kisheria pamoja na kuhuisha taarifa zake ili kuweza kutoa huduma bora za afya ya wanyama kwa wafugaji”amesisitiza
Katika hatua nyingine Dkt.Masuruli ameeleza kuwa baraza linaendelea kufuatilia huduma ya afya ya wanyama inayotolewa kwa wafugaji kwa lengo la kuboresha,kuzuia na kukinga magonjwa dhidi ya wanyama na kuongeza tija ya huduma hizo hapa nchini.