Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ameketi mbele kwenye gari aina ya Lori ambalo limeunganishwa na kiwanda hicho cha GFA kilichopo eneo la Tamko Wilayani Kibaha wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua shughuli mbali mbali zinazofanywa na kiwanda hicho ikiwa ni kuunga juhudi za Rais Dk, John Pombe Magufuli.
Meneja wa kiwanda hicho cha kuunganishia magari cha GFA Ezra akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Ebarist Ndikilo pamoja na viongozi mbali mbali waandamizi wa serikali ambao walifanya ziara kwa ajili ya kwenda kujionea shughuli mbali mbali zinazofanyika katika kiwanda hicho.
Mwonekano wa baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho cha magari cha GFA kinachojishughulisha mambo ya kuunga magari aina ya malori wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na furaha mara baada ya kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo hayupo pichani katika eneo la kiwanda hicho kilichopo eneo la Tamco mjini Kibaha.
Meneja wa kiwanda cha kuunganishia magari cha GFAEzra Mereng kushoto akimpa maelekeaoz Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua maendeleo mbali mbali pamoja na kusikiliza kero na changamoto za wawekezaji hao.
*************************************
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
SERIKALI mkoani Pwani imewataka wawekezaji mbali mbali wa ujenzi wa viwanda kuhakikisha kwamba wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa ikiwemo kulinda maslahi ya wafanyakazi wao pamoja na kuwahudumia ipasavyo hasa pindi wanapokumbwa na majanga wakiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Kauli hiyo imetolew na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa zira yake ya kikazi yeye lengo la kukagua na kutembelea baadhi ya viwanda vilivyojengwa katika Wilaya ya Kibaha ikiwemo kiwanda cha kuunganishia magari aina ya malori kinachojulikana kwa jina la GFA kilichopo eneo la Tamco Wilayani Kibaha pamoja na kusikiliza changamoto amabzo zinawakabili ili kuzifanyia kazi.
ametoa rai kwa wamiliki wa Viwanda ndani ya Mkoa huo kuzingatia haki na maslahi ya wafanyakazi wao.
Katika ziara hiyo Ndikilo alisema kwamba lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba inaendelea kuwasaidia kwa hali na mali wawekezaji wote wazalendo na wal wengine wa nkje ili kuja kuwekeza kujenga viwanda mbali m ali ambavyo vitaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwa wananachi wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani pamoja na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mhandisi Ndukilio aliongeza kuwamba kukamilia kwa ujenzi wa kiwanda hicho kutaweza kutoa fursa mbali mb ali za ajira kwa vijana kutokana na kuweza kupata kazi m ali mbali ambazo zitaweza kuwasidia kujikwamua kuchumi na kuendesha maisha yao .
“Kikubwa mimi ammbachoi ninawaomba wamiliki wa viwanda hivi pamoja na kumuunga mkoni Rais wetu katika ujenzi wa viwanda lakini ni lazima kabisa tuhakikishe kwamba tuanazingatia sheria na taratibu za kaiz kwa wafanyakazi ambao wanafanya kazi hizi kwa kuwa wanatakiwa wapatiwe stahhiki zao zote bila uonevu na kuwahudumia ipaswavyo pindi wanapohumia waakiwa kazini,”alisema Ndikilo.
Pamoja na hayo alifafanua kuwa , katika ajira mbali mbali zinazotolewa kwa wafanyakazi zinatakiwa kuendana na haki ikiwemo vitendea kazi pamoja na maslahi na Afya zao wakiwa kazini.
” Baadhi ya wamiliki hawazingatii haki na maslahi ya wafanyakazi wao, wanawajali pale wanapokuwa wazima na kufanya kazi kwa bidii wakipata matatizo hawana habari nao, niwaombe kuheshimu wafanyakazi na kuwajali muda wote wakiwa kazini na wanazokumbana na matatizo” alisema Ndikilo
Aidha mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wamiliki hao wa Viwanda kutumia benki zilizopo ndani ya mkoa huo, kupitisha fedha zao na kuomba mikopo lengo kukuxa pato la Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
Alitoa wito kwa Taasisi wezeshi za Mkoa huo kujipanga vizuri kutoa vibali kwa wawekezaji ili shughuli za Uwekezaji zifanyike kwa wakati.
Awali meneja wa Kiwanda hicho Ezra Mereng alisema Kiwanda hicho Cha kuunganishiwa magari kitakapokamilika kitakuwa na Uwekezaji wa zaidi ya bilioni 12.
Katika hatua nyingine aliongeza kuwa malengo yao ya baadae ni kuwa na ajira 300 za moja kwa moja na zisizorasmi 700 ambapo kwa sasa zipo ajira 65 pekee na kwamba wataendelea kutoa ajira nyingine zaidi kulingana na mwenenndo wa uzalishaji ambavyo utakuwa ukiongezeka.