Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati (mwenye suti ya drafti) akiangalia mmoja ya bidhaa za nyuzi zinazozalishwa na Kiwanda cha Nyuzi Tabora wakati wa ziara yake jana ya kukagua shughuli mbalimbli kiwandani humo.
Katibu wa Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora Jotham Pascal(katikati) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati (mwenye suti ya Drafti) alipotembelea kiwanda hicho jana.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati (mwenye suti ya drafti) akimwangalia mmoja wa kiwanda cha Nyuzi cha Tabora jinisi alisimamia mitambo ya kutengeza nyuzi wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi jana.
Picha na Tiganya Vincent
*********************************
NA TIGANYA VINCENT
TABORA
MAMLAKA zinazosimamia viwanda zimeombwa kuangalia uwezekano wa kuchukua hatua na kufanya maumuzi yanazostahili kwa Mwekezaji wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora kwa kushindwa kukiendesha kulingana na mkataba wake wa ununuzi ili kiwezo kuongeza uzalishaji wa kuleta tija kwa Taifa na Mkoa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati baada ya kutembelea Kiwanda hicho ili kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji wa nyuzi ya pamba kwa ajili ya masoko mbalimbali na kutoridhishwa na utendaji kazi wake.
Alisema Mwekezaji aliponunua Kiwanda hicho alitoa ahadi za kukifanyia ukarabati ili kiwe cha kisasa na kisaidie kuleta mapinduzi ya viwanda hapa nchini lakini hajatekekeza jambo hilo.
Dkt. Sengati alisema kuwa licha ya Mwekezaji huyo kukukopa fedha nyingi katika Taasisi mbalimbali kama vile kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 6.1 na fedha za kitanzania shilingi bilioni 1 hazikuwekezwa katika Kiwanda ili kionekana kinafanya kazi kwa tija.
Alisema fedha hizo zingewekeza katika Kiwanda zingeondoa matatizo mbalimbali ikiwemo uchakavu wa mitambo kwa kuleta teknolojia ya kisasa.
Dkt. Sengati aliongeza kuwa Mwekezaji huyo pia amekiuka lengo la Kiwanda la kuzalisha nyuzi kwa ajili ya kutengenezea nguo kwenye Viwanda vya nguo vya hapa nchni bali ameanza kutengeneza Kamba za kufungia mazao na vitambaa.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa Mwekezaji huyo pia ameuza mali za Kiwanda ikiwemo nyumba mbili za ghorofa na nyumba nyingine tano kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 ambapo fedha hizo hazionyesha kuboresha Kiwanda.
Alisema wakati bado kiwanda kinamilikiwa na Serikali kilikuwa na waajiriwa zaidi ya 1,000 lakini baada ya kukibinafisisha wamepungua na kubaki 100.
Dkt. Sengati alisema kutokana na mwenendo wa utendaji wa Kiwanda hicho hivi sasa inaonekana kinaendeshwa kwa hasara ni kubwa kuliko faida ambayo Serikali ilitarajia kuiona baada ya ubinafsishaji.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Tabora alisema ni jukumu la Mmiliki wa Kiwanda kupitia Idara ya Masoko kutafuta masoko na sio Serikali kama wao wanavyoomba wasaidiwe.
Awali Katibu wa Kiwanda hicho Jotham Pascal alisema baada ya kukinunua kiwanda hicho Viwanda vya nguzo ambavyo ndio walikuwa wateja wao wakubwa wa nyuzi zao walianza kuagiza toka nje na kuwadhofisha.
Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo waliamua kubadilika na kuanza kutengeneza kamba na vitambua kwa ajili ya ufungaji tumbaku na kuhifdha pamba iliyochambuliwa.
Pascal aliwaambia Mkuu huyo wa Mkoa alisema uwezo wa kuzalisha bidhaa za aina mbalimbali wanao ikiwa watahakikishiwa na kutafutiwa soko la uhakika.