Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2020/2021 hadi 2029/2030 hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja, akitoa taarifa kabla ya Uzinduzi wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2020/2021 hadi 2029/2030 hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga akizindua Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2020 hadi 2030 hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga, akimkabidhi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG), Bw. Charles Kichele Kitabu cha Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2020 hadi 2030, baada ya kuzinduliwa leo jijini Dodoma.
Sehemu ya Wadau wakifatilia uzinduzi wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2020 hadi 2030, hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mary Maganga, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mara baada ya kuzindua Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2020 hadi 2030 hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali kupitia wizara ya Fedha na Mipango imezindua mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha utakaotumika kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia 2020/2021 hadi 2029/2030 wenye lengo la kuongeza wigo na fursa za upatikanaji wa huduma za fedha kwa wananchi wote zikiwemo za bima.
Akizindua mpango huo leo jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mary Maganga kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Doto James,amesema kuwa mpango huo utaongeza wigo katika upatikanaji wa huduma za mikopo ,akiba ,uwekezaji na kuongeza mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa uchumi unaoendeshwa na sekta ya viwanda.
Bi.Maganga amesema kuwa mpango huo umeandaliwa ili utumike katika kutatua changamoto zilizopo ambapo pamoja na mambo pia umelenga kuongeza upatikanaji mitaji ya muda mrefu, upatikanaji huduma jumuishi za fedha na kulinda watumiaji wa huduma za fedha .
Pia kuimarisha uthabiti wa sekta ya fedha ,kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika sekta ya fedha ,kudhibiti utakatishaji fedha haramu na kuweka mazingira wezeshi ya sheria ,kanuni ,taratibu na miongozo katika sekta ya fedha.
Aidha amewataka waratibu na wasimamizi wa mpango huo kuwianisha mipango mbalimbali ili iendene na mpango huo Mkuu wa kitaifa katika maeneo wanayoyasimamia .
“Maeneo hayo ni katika sekta ndogo zilizomo ndani ya sekta hii ikiwa ni pamoja na benki,bima ,masoko ya mitaji na dhamana ,mifuko ya hifadhi ya jamii na sekta ya huduma ndogo za fedha.”amesemaBi.Maganga
Hata hivyo amevitaka vyuo vikuu na taasisi za utafiti amewataka kuona fursa zilizopo katika mpango huo na kujipanga katika kuboresha maeneo mbalimbali ya kitaaluma na kiutafiti ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kuwa yenye ushindani na kuweza kuhimili mabadiliko ya nyakati kwa wepesi na weledi.
Awali Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Dkt.Charles Mwamwaja amesema wakati wa maandalizi,timu ya wataalam wa Mpango huo ilifanya mapitio kwenye nyaraka mbalimbali zikiwemo taarifa za maboresho ya sekta ya fedha ,Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025,Dira ya Taifa ya Maendeleo Zanzibar ya mwaka 2020 na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza umasikini Zanzibar (ZSGRP III) .
Pia ilipitia Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2016/17-2020/21 na taarifa ya Programu ya Tathimini ya Sekta ya Fedha yam waka 2018 kwa lengo la kupata matokeo zaidi katika utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Kitaifa.