Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Watendaji wa Afya katika Halmashauri ya Kongwa wakati alipotembelea Kijiji cha Mlali kilichopo Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu bora ya vyoo kwenye Kaya za Halmashauri hiyo inayotekeleza mpango maalumu wa usafi wa mazingira (Water, Sanitation and Hygiene) (WASH).
Moja ya Mashine ya akiba ya kituo cha afya Mlali inayotumika umeme unapokuwa umekatika katika ktuo hicho.
Timu za Afya Halmashauri ya Kongwa na Mkoa wa Dodoma wakimfatilia Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima (HAYUPO PICHANI) wakati alipotembeleza Kijiji cha Mlali kilichopo Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu bora ya vyoo kwenye Kaya za Halmashauri hiyo inayotekeleza mpango maalumu wa usafi wa mazingira (Water, Sanitation and Hygiene) (WASH)
Muonekano wa Jengo la upasuaji la Kituo cha Afya Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma
Muonekano wa mashine ya kufulia nguo za hospitali katika Kituo cha Afya Mlali katika Halmashauri ya Kongwa Mkoani Dodoma
Watendaji wa Afya katika Halmashauri ya Kongwa wakimfatilia Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima (HAYUPO PICHANI) wakati alipotembeleza Kijiji cha Mlali kilichopo Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu bora ya vyoo kwenye Kaya za Halmashauri hiyo inayotekeleza mpango maalumu wa usafi wa mazingira (Water, Sanitation and Hygiene) (WASH).
…………………………………………………………………………….
Na. Majid Abdulkarim, Kongwa
Serikali imewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini kuhakikisha mashine na vifaa vyote vilivyopelekwa katika maeneo yao kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za afya vinafanya kazi ipasavyo ili kuwarahisishia kazi wataalamu na wahudumu wa afya.
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima wakati alipotembelea Kijiji cha Mlali kilichopo Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu bora ya vyoo kwenye Kaya za Halmashauri hiyo inayotekeleza mpango maalumu wa usafi wa mazingira (Water, Sanitation and Hygiene) (WASH).
Dkt. Gwajima akiwa katika ziara hiyo amegundua kuwa kuna mashine ya kufulia nguo za hospitali katika Kituo cha Afya Mlali ambayo haifanyi kazi tangu imeletwa mwaka jana hivyo amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha mashine hiyo ndani ya siku saba inaanza kufanya kazi.
“Natoa siku saba mashine hii isipofanya kazi nakuja kuihamisha na kuipeleka katika vituo vingine vilivyojengwa ili ikatoe huduma stahiki badala ya vituo hivyo nao kuanza mpango wa kununu ingine wakati hii ipo hamtumii wakati mlisema mnahitaji na Serikali ikaleta” ameisitiza Dkt. Gwajima.
Dkt. Gwajima ameeleza kuwa shida ya baadhi ya watumishi nchini wao ni kulalamika hiki au kile hakipo lakini Serikali ikishawafikishia mahitaji hayo hawasimamii kuhakikisha vifaa hivyo vinafanya shughuli zake kikamilifu.
Hata hivyo Dkt. Gwajima amewataka Timu ya Afya Wilaya ya Kongwa (CHMT) kuacha uzembe na kutekeleza majukumu yao kwa kasi na ufasaha zaidi ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa na kupatiwa huduma bora za afya katika maeneo yao.
Vilevile, Dkt. Gwajima ametoa wito kwa Kamati za Usimamizi wa Vituo vya Afya kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji na usimamizi wa karibu wa masuala yasiyo ya kitaalamu yanayohusu uongozi na matumizi sahihi ya raslimali ili kuhakikisha huduma zilizokusudiwa kila kitengo zinatolewa.
Kwa Upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Mlali Dkt. Alanus Bagambabyaki amesema njia bora ya kujifunza anayoamini ni kufanya makosa hivyo wamefanya makosa na wamejifunza.
“Kwa niaba ya wenzangu nikuhakikishie kuwa tutatekeleza maelekezo yako na yote tuliyojifunza kwa ubora unaotakiwa katika utendaji kazi”, ameeleza Dkt. Bagambabyaki.