Wananchi wa kata ya Ikongosi
wanategea kupata maendeleo makubwa kwa miaka mitano ijayo kutokana na mikakati
aliyokuwanayo mgombea udiwani wa kata ya Ikongosi Negro Sanga wakati akiomba
kura za Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania kwa kuwa yeye ameshapita bila kupigwa.
Hayo yalisemwa kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mtili kilichopo kata ya Ikongosi kwa
kutoa ahadi ya kukamilish ujenzi wa ofisi ya kata kwa kuwa kila kitu kipo
kwenye mipango dhabiti kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo.
Sanga alisema kuwa wanatarajia
kuwa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi itajengwa katika kata ya Ikongosi kwa
kuwa mchakato wote ulishafanyika kwenye baraza la madiwani lilolopita hivyo
wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa zitakazo jitokeza hapo baadae.
Alisema kwa miaka mitano
iliyopita maendeleo mengi na makubwa yamefanyika katika kata hiyo kwenye sekta
ya afya,miundombinu kama barabara,majengo,sekta ya michezo,elimu,kilimo na
biashara hivyo wananchi wametakiwa kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi kwa
utekeleza wa Ilani yake.
“Miaka mitano mliyonipa ridhaa
ya kuwa diwani wenu kwa ushirikiano mkubwa tumefanya kazi kubwa ya kujenga
Ofisi za vijiji kwenye vijiji vyote vitano tena kwa ubora mkubwa na sasa kwa
pamoja tunatekeleza ujenzi wa ofisi ya kata” alisema Sanga
Aidha Sanga alimuomba mgombea
ubunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe kutengeneza ushirikiano
ulitukuka kwa wabunge zenzake wa wilaya ya Mufindi kwa lengo la kusaidiana
kuleta maendeleo kwenye wilaya ya Mufindi ambavyo inautajili mkubwa.
Mgombea udiwani huyo alimalizia
kwa kumshukuru mbunge aliyemaliza muda wake Mahmoud Mgimwa kwa ushirikiano wa
kimaendeleo alioutoa kwenye kata hiyo kwa kipindi chote alichokuwa madarakani
kwenye jimbo la Mufindi Kaskazini.
Kwa upande wake mgombea ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazinikupitia Chama cha Mapinduzi
(CCM),Exaud Kigahe alisema kuwa jimbo laMufindi Kaskazini linakabiriwa na
changamoto ya miundombinu ya Barabara ambazozimekuwa hazipitiki kwa msimu mzima
hivyo akipewa ridhaa ya kuwa mbungeatahakikisha anatatua kero hiyo.
Alisema kuwa atahakikisha anaboresha sekta ya Elimu kwa kujenga na kukarabati
majengo ya shule,kuanzisha mashindano ya kumpata mwananfunzi bora namwalimu
bora kwa atakayefanya kazi nzuri ya kuwasaidia wanafunzi kufaulu kwawastani
mzuri.
“Wananchi wa jimbo la Mufindi wengi niwakulima hivyo siwezi kuisahau sekta ya
kilimo kwa kuwa hata mimi nimekuliakwenye family ya wakulima hivyo
nitahakikisha kuwa tunaboresha masoko ya wakuliwa ili waweze kuuza mazao yao
kwa bei nzuri” alisema Kigahe
Aidha Kigahe alisema kuwa ahadi nyingine ni pamoja na
viwanda,afya,biashara,umeme na michezo ambazo atazifanyia kazi kama akiwambunge
wa jimbo la Mufindi Kaskazini.
“Kazi kubwa mliyonipa nitaifanya kwa nguvu naniwahakikishie sisi wabunge watatu
wa Wilaya ya Mufindi (Kihenzile na Chumi) tutafanya kazi kwa pamoja kwa kuwa
lengokubwa ni kuleta maendeleo”alisema Kigahe