Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko, akifungua warsha ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 11 Jijini Dodoma, kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi akieleza umuhimu wa wadau kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, wakati wa kikao kazi ikilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia kikao kazi kilicholenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, warsha hiyo imeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia kikao kazi kilicholenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, warsha hiyo imeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Mratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jumanne Gomera, akiwasilisha wasilisho la taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, wakati wa warsha ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma kujadili taarifa hiyo, kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia Warsha iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi na Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje wakiteta jambo wakati wa kikao kazi cha wadau wa uwekezaji sekta ya Umma iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji imekutana na wadau wa uwekezaji wa sekta ya Umma kwa lengo la kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996. Wadau hao ni kutoka Wizara, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali. Baada ya kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera hiyo,wameridhishwa kwa jinsi ilivyobainisha nchi inavyoweza kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje.
Wakipongeza wakati wa kujadili taarifa hiyo, leo tarehe 11 Septemba, 2020 jijini Dodoma. Wadau hao wamesisitiza Tathmini hiyo iliyojikita kwenye masuala ya kisera, kisheria na kiutendaji inaendelea kutoa mapendekezo ya kuendelea kutatua changamoto za uwekezaji nchini hususani kwenye maeneo ya Uratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Utangazaji wa Fursa za Uwekezaji, Uwezeshaji Uwekezaji, pamoja na Vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi.
Akiongea wakati akifungua kikao kazi hicho, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Bibi Dorothy Mwaluko amesisitiza kuwa upo umuhimu wa wadau hao kubainisha masuala ya kisera, kiutendaji na kisheria, ili kuhakikisha kuwa Sera ya Taifa ya uwekezaji na Sheria ya Uwekezaji nchini haikinzani na sheria nyingine za kisekta kwenye masuala ya uwekezaji.
“Serikali imekuwa ikitunga Sera na Sheria kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara nchini, tunahitaji kuwa na Sera madhubuti za kuvutia na kuwezesha uwekezaji katika sekta zote ili kutumia vilivyo fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.”Amesisitiza Mwaluko.
Akiongea kwenye kikao kazi hicho Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje, amefafanua kuwa kukutana kwa wadau hao kujadili taarifa ya tathmini hiyo kutawezesha kujua changamoto wanazozipata wakati wa utekelezaji wa sera hiyo na hatimaye utatuzi wake, utawezesha uwekezaji na kuleta tija kwa mwananchi wa kawaida.
Naye Mkurugenzi wa Uwezeshaji Uwekezaji, kutoka Mamlaka ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje (EPZ), James Maziku amefafanua kuwa, sera hiyo imetungwa kwa muda mrefu hivyo tathmini hiyo itasaidia kuhuisha (Review) Sera na Sheria za uwekezaji za kisekta, kupunguza migongano ya kiutendaji na kuelewa namna ya kuboresha utendaji wa pamoja wa kisekta.
Sera ya Taifa ya Uwekezaji imebainisha malengo mahsusi sita (6) na malengo nane (8) ya kisekta. Baadhi ya malengo hayo ni kuhamasisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje; Kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi; Kuhimiza na kuvutia matumizi ya teknolojia za kisasa katika uwekezaji; Kuweka mfumo mzuri na wa wazi wa kisheria; na kuondoa urasimu katika taratibu za upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.
Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996 na Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1997 iliyoanzisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), vinaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara za kisekta, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali. Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimepewa jukumu la kuratibu, kuvutia, kutangaza na kuwezesha wawekezaji hapa nchini.