***********************************
NJOMBE
Kituo cha Forodha ya Makambako kwa kushirikiana na jeshi la polisi kimeteketeza vipodozi feki vyenye thamani ya zaidi ya mil 200 vilivyoingia kimagendo nchini vikitokea nchi jirani ya Zambia.
Vipodozi hivyo vilikamatwa 2017 mara baada ya raia wema kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama kuwa kuna gari ya mafuta imebeba mzigo huo kinyume cha taratibu ikijaribu kuingiza nchini.
Akizungumza wakati wa zoezi la uteketezaji wa vipodozi hivyo Meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Njombe Shaban Musibu na Odero Ryoba mkuu wa forodha ya Makambako wanasema endapo vipodozi hivyo vingeingia sokoni vingekuwa na athari kwa watumia na serikali kwa kukosa mapato.
Musib amesema kuingiza bidhaa kinyemela ni kinyume cha sheria na kwamba endapo mtu anabainika kufanya hivyo bidhaa iliyokamatwa inatekezwa kwa mujibu wa sheria ya ushuru wa forodha ya 2004 ya africa mashariki .
” Kitendo cha kuingiza bidhaa nchini kinyemela kinafanywa na wafanyabiashara wenye lengo la kujinemesha na kukwepa kulipa mapato ya serikali”Alisema Musib
Paul Malala ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako ambao ndiyo kitovu cha biashara katika mkoa wa Njombe anasema kitendo cha kudhibiti tani 2 za vipodozi feki kuaokoa maisha ya wengi na kuzitaka mamlaka za ukaguzi kukagua maduka yote mjini hapo feki ambazo zinaweza kusababisha athari kiafya kwa watumiaji”Alisema Paul Malala.
“Niwatake mamlaka mbalimbali za ukaguzi kuhakikisha zinakagua bidhaa zote madukani ili kubaini zilizoingia kinyume cha taratibu”Alisema Paul Malala.
Kwa upande wake Frola Nyato ambaye ni afisa tarafa makambako kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri analazimika kutoa onyo kwa wafanyabiashara wajanja wajanja na wananchi hutumia bidhaa ambazo zimeingia kinyume cha taratibu huku akiwataka kuripoti katika vyombo vya mamlaka