TUKIO LA KWANZA.
TAREHE 08.09.2020 MAJIRA YA 22:00HRS HUKO MAENEO YA KAYENZE, KATA YA KAYENZE, WILAYA YA ILEMELA, MKOA WA MWANZA, MTOTO AITWAYE VERONICA ANTHONY, MIAKA 17, MSUKUMA, MWANAFUNZI DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI KAYENZE, MKAZI WA ISENI, ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYE ANTHOY COSTANTINE @ MANINGU, MIAKA 50, MSUKUMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ISENI, BAADA YA KILE KINACHODAIWA KURUDI NYUMBANI KWAO AKIWA AMECHELEWA MAJIRA YA USIKU KITENDO KILICHO KINACHODAIWA KUMKASIRISHA BABA YAKE MZAZI NA KUAMUA KUTOA ADHABU YA KIKATILI KWA BINTI YAKE ILIYOPELEKEA MAUAJI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA UCHUNGUZI WA DAKTARI. MTUHUMIWA AMBAYE NI BABA MZAZI WA MAREHEMU AMEKAMATWA NA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA ZA KISHERIA.
TUKIO LA PILI;-
TAREHE 09.09.2020 MAJIRA YA 01:00HRS HUKO MAENEO YA MHONZE “A”, KATA YA SHIBULA, WILAYA YA ILEMELA, MKOA WA MWANZA, EMMANUEL JOSEPH, MIAKA 49, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA MHONZE ‘A”, ALIUAAWA BAADA YA KUPIGWA NA KITU KIZITO UTOSINI NA NDUGU YAKE MUSSA GABRIEL @ MAJUTO, MIAKA 35, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA MHONZE
INADAIWA MAREHEMU ALIKUA AKIMTUHUMU MTUHUMIWA KUMWIBIA SIMU YAKE AINA YA TECNO YA BATANI YENYE THAMANI YA TSH 40,000/=. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA YA SEKOU TOURE KWA UCHUNGUZI WA DAKTARI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA UPELELEZI UNAKAMILISWA NA ATAFIKISHWA MAHAKANI HARAKA IWEZEKANAVYO
TUKIO LA TATU
TAREHE 09.09.2020 MAJIRA YA 19: OOHRS KATIKA KIJIJI NA KATA YA ILULA, TARAFA YA NYAMILAMA, WILAYA YA KWIMBA, MKOA WA MWANZA, MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA ANTHONY ANAYEKADIRIWA KUWA NA MIAKA 25 -27, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA MABUKI, KWA MAKUSUDI ALIBANDUA BANGO LENYE PICHA YA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KWIMBA KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI NDUGU SHARIFU MANSOOR NA KULICHANA. KITENDO HICHO NI KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI. MTUHUMIWA ATAKAMATWA NA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA WITO KWA WAZAZI, WALEZI NA FAMILIA KWA UJUMLA KUWA MAKINI NA ADHABU WANAZOTOA KWA WATOTO KWANI ZINAWEZA KUWAPELEKEA KUTENDA UKATILI DHIDI YA WATOTO NA KULETA MADHARA MAKUBWA KATIKA FAMILIA NA BAADAE KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA JINAI. PIA POLISI ITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA KALI ZA KISHERIA WATU WOTE WASIOHESHIMU SHERIA ZA NCHI NA KUTAKA KUVURUGA ZOEZI ZIMA LA UCHAGUZI MKUU KWA AINA YOYOTE .
IMETOLEWA NA;
Muliro JUMANNE MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
10 SEPTEMBA, 2020