Na John Walter-Manyara
Wakati kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani zikiendelea kote nchini, Jeshi la Polisi mkoani Manyara limeeleza kuwa limejipanga kusimamia hatua zote ili Uchaguzi huo ufanyike kwa Amani, Huru na Haki.
Kamanda wa Jeshi Polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago amesema katika mkoa huo hakuna matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa hadi sasa vyama vyote vinaendelea kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutoa sera kwa wananchi ili kuwashawishi kuwachagua.
Kasabago amewaambia waandishi wa habari kuwa mpaka sasa hakuna Chama cha Siasa kilichoripoti kufanyiwa fujo au kutumia lugha ya Matusi.
Kamanda Kasabago ametoa wito kwa Wanasiasa kuendelea kufanya siasa safi na kuwa wastaarabu ili waweze kutoa sera zao.
Vyama vyote vya Siasa vinaendelea na kampeni kunadi sera zao kwa wananchi ili kupewa ridhaa ya kuongoza Kata,Jimbo na Nchi ifikapo Oktoba 28,2020.
Attachments area