NA DENIS MLOWE,IRINGA
MASHINDANO ya soka kugombea kombe la Ngajilo yaliyokuwa yazinduliwe rasmi Machi 22 na kuahirishwa kutokana na kuunga mkono kauli ya serikali iliyotolewa na waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa katika kupambana na virusi vya gonjwa hatari la Corona yanafunguliwa leo September 5 kwenye viwanja vya shule ya msingi Mlandege.
Akielezea mashindano hayo , Mratibu wa mashindano hayo, Davis Wapalila alisema kuwa taratibu zote za kuanza mashindano hayo zilikwishakamilika na timu shiriki zinatakiwa kufika eneo la tukio kuanzia saa Saba mchana wa Leo kuweza kufanikisha zoezi la ugawaji wa jezi na vifaa kwa timu shiriki.
Alisema kuwa baada ya zoezi la kufanya usajili kwa kila timu shiriki kumalizika kilichobaki na kuanza kwa mashindano hayo ambapo mechi ya ufunguzi Itakuwa Kati ya wapinzani wa Jadi Kitanzini FC na Mshindo fc
Alisema kuwa timu ambazo zilitarajia kushiriki mashindano hayo ni 32 lakini zilizorudisha fomu ni timu 16 ambazo zitagaiwa jezi na mpira kwa ajili ya mashindano hayo yanayosubiriwa kwa hamu kubwa mkoani hapa.
Alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa na zawadi nono kwa timu bingwa ambapo Kila timu shiriki itapata jezi seti 1 na mpira mmoja kabla ya mashindano kwa ajili ya maandalizi.
Alisema kuwa bingwa wa mashindano hayo mwaka huu ataondoka n ash.Tshs 1,000,000/ na Kombe la Ubingwa , ambapo mshindi wa pili Tshs 500,000/ na mshindi wa tatu ataondoka na Tshs 300,000/.
Wapalila alisema kuwa zawadi nyingine ni kwa timu yenye nidhamu ambapo itajipatia Jezi seti moja, Mchezaji bora wa mashindano, Mwandishi bora wa Radio kipindi cha michezo, Mwandishi bora gazeti upande wa michezo, blogs na mwamuzi bora wataoondoka na zawadi ya sh,70,000 huku Mfungaji bora na Mwamuzi bora msaidizi watajipatia 50,000
Kwa upande wake mdhamini wa mashindano hayo, Fadhili Ngajilo alisema kuwa kuanzishwa kwa mashindano hayo ni fursa kubwa kwa vijana wote bila kutazama vyama vyao kushiriki kutangaza vipaji vyao ili timu mbali mbali kupata wachezaji kupitia mashindano hayo ambayo wamewashirikisha viongozi mbali mbali wa timu kubwa za mkoa wa Iringa kufika kusajili wachezaji .