Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Ikungi mkoani Singida wakati akielekea Singida mjini kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa Chama cha Mapinduzi CCM
Wananchi wa Ikungi mkoani Singida wakimshangilia Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili wakati akitokea Wilaya ya Bahi kwenye Mikutano ya Kampeni za Urais.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiandika jambo katika hotuba yake kabla ya kuanza kuzungumza na Wananchi wa Ikungi mkoani Singida. (PICHA NA IKULU)
…………………………………………
Na. Majid Abdulkarim, Ikungi
Uongozi wa halmashauri ya Wilaya Ikungi umepewa miezi miwili kuwa umekamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi ili wananchi waweze kupatiwa huduma katika hospitali hiyo.
Agizo hilo limetolewa na Mgombea Urais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli leo wakati wa komba kura akiwa njiani wilayani Ikungi kuelekea Singida.
Aidha Dkt. Magufuli amesema kuwa baada ya miezi miwili aliyowapa ongozi wa wilaya hiyo ataenda kuzindua hospitali hiyo ili ianzekutoa huduma kwa wananchi wa Ikungi na watanzania kwa ujumla.
Dkt. Magufuli amesema kuwa ili kuendelea kusonga mbele anaomba kura za ndio pale itakapofika siku ya kupiga kra ili akakamilishe akusimamia miradi alioianzisha na kuleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla.
“Hivyo basi wanaIkungi nyote na watanzania kwa Ujumla tujitathimi kwa kuangalia wapi tulipotoka, tulipo sasa na wapi tunaelekea na kfanya uamuzi sahihi wakati wa kupiga kura utakapofika 28 Oktoba,2020”, amesema Dkt.Magufuli.
Lakini pia Dkt. Magufuli ameeleza kuwa ndani ya miaka mitano aliowatumikia watanzania kwa wilaya ya Ikungi ameweza kujenga zahanati 4,kwa kiasi cha shilingi Milioni 830,vituo vya afya viwilikwa kiasi cha shilingi milioni 900 na jenzi wa Hospitali ya wilaya unaendelea.
Hata hivyo Dkt. Magufuli ametoa wito kwa kwa wanaikungi na watanzania wote kjenga na kulinda amani waliyonayo ili kuendelea kujenga nchi kwani bila amani hakuna maendeleo.