Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la wafanyakazi wa taasisi hiyo hafla hiyo ilifanyika katika Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mwenyekiti Baraza la Wafanyakazi akizungumza katika uzinduzi wa Baraza jipya la wafanyakazi wa taasisi hiyo hafla hiyo ilifanyika katika Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Katibu TUGHE mkoa wa Dodoma akimshukuru mgeni rasmi (hayupo pichani)baada ya kuwazindulia Baraza jipya la wafanyakazi wa taasisi hiyo hafla hiyo ilifanyika katika Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Sehemu ya Baraza jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa wakifuatilia uzinduzi wa baraza hilo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula ambaye alikuwa mgeni rasmi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza Jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (katikati) akiangalia kitabu cha muongoza mara baada ya kuzindua Baraza Jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Dkt.Alphonce Chandika baada ya kuzinduliwa kwa Baraza Jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi cheti Afisa Utumishi-Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Muadhi Mayunga baada ya kuzinduliwa kwa Baraza Jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi cheti Kaimu Mwenyekiti wa TUGHE Hospitali ya Benjamini Mkapa,Benjamini Babere baada ya kuzinduliwa kwa Baraza Jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula(katikati) waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na watendaji mara baada kuzindua Baraza Jipya la wafanyakazi wa taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa jijini Dodma.
PIcha na Alex Sonna-Fullshangweblog
……………….
Na.Alex Sonna,Dodoma.
TAASISI ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa imeunda na kuzindua Baraza jipya la wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambalo limeundwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo, ambayo ni miongoni mwa hospitali kubwa hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, amewataka wafanya kazi wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa uadilifu na kujituma sambamba na kuwa wazalendo, na kuwajali wagojwa.
Dkt Chaula amesema kazi ya utabibu na udaktari ni ya neema na Rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na inayohitaji kuwa na uvumilivu , huruma na maneno ya Faraja kwa Wagonjwa hivyo kila Mmoja anatakiwa kuguswa pindi anapotoa huduma kwa mgonjwa.
“Tunajifunza kila siku,kwa hiyo nyie mlioteuliwa mtuwezeshe,haki haipo bila wajibu,na kila mmoja akijituma atatizimiza wajibu wake,mimi sikumbuki kutumwa na napata shida kum-push mtu,na lazima tutengeneze Mechanism ya watu kufanyakazi bila kutumwa”
“Hakuna kazi ya neema na ibada tunayo fanya kama hii,Mtu ana Stress zake,ana shida,hana hela lakini unamfariji,unamtibu,mwisho wa kazi saa 9 ukifanya kazi mpaka saa 11 au saa 1 jioni una dhambi gani.”Amesema Dkt Zainabu.
Mwa upande mwingine, Dkt Chaula amewataka wafanyakazi kuwa Wepesi katika kutekeleza Majukumu yao na kutowakwaza wagonjwa na wananchi kwa ujumla hivyo ni jambo la busara kupeana Moyo katika kazi ngumu na yenye wito ya utabibu na kumtegemea Mungu katika changamoto wanazokumbana nazo .
“Kwa makusudi tu mtu anakuja halafu anatoka analia ofisini kwako unajisikiaje,lazima tupendane tuhurumiane tukitengeneza system ya namna hii katika maisha yetu tutakuwa na marafiki wengi kuliko maadui,tusameheane” Amesema.
Kwa upande wake Katibu wa Baraza la wafanyakazi mkoa wa Dodoma,ambaye pia Mjumbe Taifa wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali kanisa la Waadventista Wasabato ,[ATAPE] Bw.Mchenya John, amesema wataendelea kuyafanyia kazi na maelekezo yote muhimu yaliyotolewa.
Na kuzungumzia namna walivyofanya mchakato wa uanzishaji wa Chuo kikuu cha Dodoma pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa akitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha uanzishaji wa Hospitali hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa ambaye pia mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt Alphonce Chandika amesema taasisi hiyo ina takriban miaka mitatu tangu ianzishwe.
Na amebainisha kuwa walikuwa hawajaunda Baraza la Wafanyakazi kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wafanyakazi kutokujitosheleza lakini kwa sasa idadi imejitosheleza na wameona kuwa na umuhimu wa kuwa na Baraza ambapo tayari na katiba na mkataba wa Baraza hilo ilishatengenezwa.