Meneja wa Usajili,Ukaguzi na Udhibiti wa Usalama wa Vyombo vya maji Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Afred Waryana wa pili kushoto akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alipotembelea banda lao wakati wa maadhimisho ya wiki ya mabaharia kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
Sehemu ya mabaharia wakiwa kwenye warsha hiyo
Sehemu ya mabaharia wakiwa kwenye warsha hiyo
Sehemu ya wanafunzi wa shule za Sekondari wakiwa kwenye warsha hiyo
UKAGUZI wa kushtukiza mara kwa mara kwenye vyombo vya majini umeelezwa kwamba unaweza kusaidia kuondosha vyombo vya majini visivyokuwa na ubora na hivyo kusaidia kupunguza majanga yanayoweza kujitokeza wakati wakiendelea kutoka huduma hizo ikiwemo meli
Hayo yalisemwa na Meneja wa Usajili,Ukaguzi na Udhibiti wa Usalama wa Vyombo vya maji Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Afred Waryana wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo mabaharia na wadau wa masuala ya usafirishaji wa majini iliyoandaliwa na shirika la hilo kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi.
Alisema kwamba wanafanya hivyo ili kuhakikisha meli zinazofanya kazi na kutoa huduma majini wamiliki wake wanafuata taratibu na viwango vinavyostahili ikiwemo kuwa na ubora ili kuweza kuepusha majanga ambayo yanaweza kujitokeza wakiwa wanaendelea na shughuli hizo.
“Tumekuwa tukifanya kaguzi mbalimbali kwa lengo la kujirihidhisha na ubora wa meli husika na hili hufanyika wakati wa meli inajengwa kabla ya kuingizwa majini, ukaguzi wa kila mwaka kuhakikiwa kwamba ina ubora”Alisema
Aidha alisema pia wamekuwa wakifanya ukaguzi wa kila baada ya miaka miwili na nusu kwa meli kutolewa kwenye maji na kuangaliwa kama bado ina viwango hiyo yote ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha vyombo vya majini vinavyotoa huduma majini vinakuwa na ubora unaotakiwa.
Mkurugenzi hiyo alisema kwamba kaguzi hizo zipo kwa mujibu wa sheria lengo likiwa ni kuhakikisha meli hazitoi huduma bila kukaguliwa huku akieleza wanafanya za kushtukiza kuzuia watu kufanya shughuli za meli bila kukaguliwa.
Alisema kwa sasa wanafanya ukaguzi kwa vyombo 6000 vya majini nchi nzima kwa kila mwaka huku vyombo vikubwa meli kubwa na ndogo vilivyo zaidi ya tano 50 kwenda juu wanakagua zaidi ya kaguzi 230.
Awali akizungumza wakati akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo Captain Hilaly Salum kutoka Chuo cha Mabaharia (DMI) Dar es Salaam akiwasilisha mada ya tatu katika Warsha hiyo alikieleza chuo hicho pekee Afrika Mashariki kilichoanzishwa miaka 42 iliyopita kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kiteknolojia na hali ya kiuchumi.
Alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali na taasisi kukisaidia chuo hicho kupata vyombo kwa ajiri ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ambavyo vitawawezesha kufanya majaribio wasifu pamoja na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa ngazi ya chini ambao hawana uwezo kugharamia masomo hayo.
“Endapo serikali itagharamia elimu hiyo kwa wanafunzi wa chini wasiyo na uwezo kifedha wa kulipa ada licha ya kuwafanya kupata ajira lakini pia watailipa serikali kodi na hivyo kuchangia uchumi wa taifa”alieleza Salimu.
Awali wakichangia mjadala baadhi ya washiriki wa warsha hiyo waliiomba serikali kufanya uwekezaji katikamazao ya baharini kama inavyofanya kwenye sekta mbalimbali nchini na kwamba kufanya hivyo kutaongeza pato la taifa kwa madai kuwa bahari ndiyo eneo pekee lenye uwezo mkubwa wa kufanya uwekezaji Duniani.