Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wananchi wa kijiji cha Rungemba wakati wa ziara ya kukagua miradi pamoja na kusikiliza kero za wananchi
Stephen Kalinga akiwa kwenye gari ya polisi baada ya mkuu wa mkoa kuamuru akamatwe kwa kosa la kuongea uongo kwenye mkutano wa hadhara
Stephen Kalinga na mwenzake wakiwa kwenye gari ya polisi baada ya mkuu wa mkoa kuamuru wakamatwe kwa kosa la kuongea uongo kwenye mkutano wa hadhara
Mgunda,Iringa.
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Ally Hapi ameamuru kukamatwa kwa mwenyekiti wa bodi ya maji ya
kijiji cha lungemba wilayani mufindi Stephen Kalinga kwa kosa la kuwa
mchonganishi baina ya serikali na wananchi huku akiahidi kuchangia mifuko 100
ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa wodi la akinamama.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kukagua miradi halmashauri ya Mji wa Mafinga katika zahati
ya kijiji cha Rungemba, mkuu wa mkoa alibaini kuwepo kwa tuhuma ambazo hazina
ukweli wote.
Akisikiliza
kero za wananchi wa kijiji hicho,mkuu wa mkoa alipokea barua kutoka kwa
mwananchi iliyokuwa inatuhuma kwa baadhi ya viongozi wa kijiji hicho na kuanza
kuzitafutia majibu kwa viongozi waliokuwa wametajwa.
Baada ya
kubaini kuwa ndugu Stephen Kalinga alitoa tuhuma ambazo zilikuwa hazina ukweli
kwa baadhi ya viongozi wa kijiji hicho ndipo alipoamuru kukamatwa kwa mwananchi
huyo ili aende kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.
Lakini
mkuu wa mkoa Ally Hapi alimvua cheo cha kuwa mwenyekiti wa kamati ya maji ya
kijiji hicho na kuteua kiongozi mwingine wa muda hadi pale mkutano wa kijiji
utakapopitisha jina la kiongozi mpya.
Hata hivyo
viongozi wa kijiji kijiji hicho na wananchi walimuunga mkono mkuu wa mkoa wa Iringa
Ally Hapi kwa uamuzi wa kumvua vyeo bwana Stephen Kalinga kwa kuongea uongo
ambao ulitaka kuvuruga amani ya wananchi wa kijiji cha Rungemba.
Aidha
Hapi alitoa ahadi ya kuwa kutoa mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi
wa jingo la hodi ya akina mama ikiwa ni kuunga mkono juhudi ambazo zinafanywa
na wananchi wa kijiji cha Rungemba kuleta maendeleo na kuboresha sekta ya afya.
Hapi
aliongeza kwa kusema kuwa wananchi watakiwa kuendelea kujitolea katika shughuli
za kimaendeleo kama kuiboresha zahanati hiyo hadi kufikia hadhi ya kuwa kituo
cha afya lengo kuu likiwa ni kuendelea kuboresha sekta ya afya.
“Naomba wananchi
wengine wa moa wa Iringa kuiga mfano wa wananchi wa kijiji cha Rungemba kwa
jitihada zao wanazozifanya kuhakikisha wanafanya shughuli za kimaendeleo
kijijini kwao” alisema Hapi