MKUU WA MASOKO KUTOKA ZANTEL SAKYI OPOKU AKITOA ZAWADI WA MSHINDI WA WATOTO JOEL CHRISTOPHER KATIKA MASHINDANO YA MWISHO WA MWEZI WA MWEZI YA LIYOFANYIKA LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM PICHA NA KAPTENI SELEMANI SEMUNYU.
MKUU WA MAJESHI MSTAAFU JENERALI GERGE WAITARA (ALIYENYOOSHA MKONO) AKIWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WENZIE WA MCHEZO WA GOLF WAKATI WA MASHINDANO YA MWISHO WA MWEZI YA ZANTEL PICHA NA KAPTENI SELEMAANI SEMUNYU.
******************************
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRKIANO WA AFRIKA MASHARIKI Dkt. DAMAS NDUMBARO AMEIPONGEZA KLABU YA GOLF YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA KUTOKANA NA UMAHIRI WAKE.
AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUHITIMISHA MASHINDANO YA MWISHO WA MWEZI YA ZANTEL MONTHLY MUG YALIYOFANYIKA LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM NAIBU WAZIRI NDUMARO AMESEMA UWEPO WA LUGALO NDIO MSINGI WA MAFANIKIO YAA MCHEZO WA GOLF NCHINI TANZANIA.
KWA UPANDE WAKE MWAKILISHI KUTOKA TIMU YA WAZEE KLABU YA GENERALS TEAM DKT EDMUND MNDOLWA AMESEMA SASA NI WAKATI KWA WADAU KUINGA MKONO LUGALO ILI KIWE KIWANJA BORA NCHINI NA AFRIKA MASHARIKI NA INAWEZEKANA KUTOKANA NA UIMARA WA UONGOZI ULIOPO CHINI YA JWTZ.
KWA UPANDE WAKE MWAKILISHI KUTOKA ZANTEL WALIODHAMINI MASHINDANO HAYO SAKYI OPUKI AMESEMA HUO NI MWANZO WANAAMINI WATAINGIA KATIKA MASHINDANO MAKUBWA.
KATIKA MASHINDANO MSHINDI DIVISHENI A NI MICHAEL MASAWE ALIYEPATA NET YA 71 WAKATI DIVISHENI B NI ENRY SENGEU ALIYEPATA NET YA 68 HUKU DIVISHENI C NI KHARID SHEMNDOLWA ALIYEPATA NET YA 69 HUKU KWA SENIOR MSHINDI NI NADA MARGWE ALIYEPATA NET YA 67 .
KWA UPANDE WA WANAWAKE MSHINDI NI GLORY NJANGE ALIYESHINDA BAADA YA KUFUNGANA KWA MIKWAJU YA JUMLA NET YA 66 DHIDI YA SARA DENIS.