Afisa Mtendaji kata ya Kilimani Fatuma Anti akimkabidhi fomu kugombea udiwani kata ya Kilimani kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Diwani Mteule wa chama hicho Neema Mwaluko
………………………………………………..
Na Baranabas Kisengi, Dodoma.
Diwani mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya kilimani jijini Dodoma Neema Mwaluko leo agost 19 2020 amechukuwa fomu ya kugombea udiwani wa Kata ya kilimani kupitia chama cha mapinduzi ccm Kata ya kilimani majira ya saa nne asubuhi katika ofisi za Kata ya kilimani jijini dodoma
Awali akikabidhi fomu za Tume ya Uchaguzi Afisa Mtendaji wa Kata ya kilimani Fatuma Anti amemwelekeza mgombea wa udiwani kupitia chama cha mapinduzi kuhakikisha anazisoma fomu kwa umakini na kuzijaza kwa maelekezo yaliyo elekezwa katika fomu hizo kwa uadilifu na umakini.
Fatuma amemtaka diwani huyo pindi atakapokuwa anazirejesha fomu hizo aambatanishe na picha zake nne za pasipot size na risiti ya malipo ya benk na kuhakikisha anarudisha fomu kwa muda alioelekezwa.
Kwa upande wake katibu Kata wa Chama cha Mapinduzi Kata ya kilimani Rotta Ndimbo akizungumza na wanachama waliomsindikiza diwani huyo amewaambia wanachama wa ccm kuhakikisha wamevunja makundi na kuwa na kundi moja la kilimani na diwani neema mwaluko katika kuelekea kwenye kampeni zitakazo anza hivi karibuni ma kuwataka wawae na ushirikiano kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo
Naye Neema mwaluko amewashukuru wanachama wa Kata hiyo kwa kumpatia ushirikiano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na kuwapongeza kwa kumwamini tena kupeperusha bendera ya ccm tena kwa kipindi hichi tena cha miaka mitano ya 2020-2025
Aidha Mwaluko amekishukuru chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya tawi Kata wilaya na Mkoa kwa kuweza kumwamini huku wanachama wa Kata ya kilimani kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi wa kampeni za chama hicho kitaifa utakaofanyika agost 28 mwaka huu katika viwanja vya jamuhuri ambapo zitazinduliwa na mwenyekiti taifa Dr John pombe magufuli akiwa na mgombea mwenza