Waziri Mkuu wa Tanzanzia kulia Kassim Majaliwa akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Bhakhera wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja Wilayani Bgamoyo kwa ajili ya kujionea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha sukari pamoja a shamba la miwa, kushoto kwake mwanzo ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kushoto akipatiwa maelekeza ya kina kuhusu shamba la miwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Bakresa Group Abubakari Bhakhresa ambaye yupo kilia aliyenyoosha mkono wakati walipofanya ziara yake ya kikazi kukagua maendeleo ya mradi huo wa kiwanda pamoja na shamba hilo.
Viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na watendaji wa kampuni ya Bhakhera wakiwa na Waziri mkuu wa Tanzanzia ambaye yupo katika kati yao wakibadilishana mawazo mara baada ya kutembelea kiwanda hicho cha kuzalisha sukari sambamba na kutembelea maeneo mbali mbali ikiwemo shamba kubwa na miwa.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa salamu kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali, viongozi wa kampuni ya Bhakhesa wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kukagua ujenzi wa kiwanda cha sukaari pamoja na kukagua shambala miwa .
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza katika mkutano na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari pamoja na wafanyakazi wa shamba la miwa, sambamba na viongozi wengine mbali mbali wa serikali wakiwemo kamati ya ulinzi ya Mkoa wa Pwani wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja Wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa akizungumza jambo mbela ya Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa hayupo pichani wakati alipofanya ziaara yake ya kukaguaa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha sukari.
Mkurugenzi wa benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania TADB Japhet Justin naye akitoa taaarifa fupi kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Waziri Mkuu kuhusu ushiriki wao katika kuwasaidia wakulima katika kuwawezesha kiuchumi ili waweze kufikia malengo yao.(Picha zote na Victor Masangu)
……………………………………………………………………………….
VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameridhishwa na uwekezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kulichopo eneo la Lazaba Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani na kusema kubainisha kwamba pindi utakapokamilika utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa Taifa laTanzania kuondokana kabisa na changamoto ya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kwani wakati mwingine uingizwaji huo kwani kunaweza kuwaletea madhara kwa wananchi ya kiafya.
Majaliwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja Wilayani Bagamoyo ya kukagua mradi wa ujenzi wa kiwanda cha sukari pamoja na kujionea shamba kubwa la miwa ambao uwekezaji huo unafanywa na mwekezaji mzawa kutoka makampuni ya Bhakresa na kubainisha kwamba nia ya serikali ni kungeza kasi ya kuwa na mashamba zaidi ya miwa pamoja na viwanda ambavyo vitasaidia kukuza uchumi wa nchi na kuondokana na tatizo la uhaba wa sukari kwa wananchi.
“ Ipo hatari sana tusije kuletewa vitu vitamu kutoka nje ya nchi alafu mwisho wa siku vinakuja kutuletea madhara makubwa kwa hivyo kwa sasa sisi kama serikali tunaelekeza nguvu zetu katika kuendelea kuongeza viwanda vingine vya sukari ambavyo vitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutatua tatizo la uhaba wa sukari hapa nchini.”alisema Majaliwa.
Aidha Majaliwa alisema kwamba ana imani endap kiwanda hicho cha bagamoyo sugar kitakapokuja kukamilika kitaweza kuwa ni msaada mkubwa katika ssuala zima la upatikanani wa sukari kwa kushirikiana na viwanda vingine vitano vilivyopo katika maeneo mb ali mbali ya Tanzania vikiwemo vya mtibwa sugar kilombero sugara pamoja na Kagera Sugar ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa uwepo wa bidhaa hiyo ya sukari.
Pia Majaliwa alisema kwamba nia ya serikali ni kuona wananchi wake wanaondokana na changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo ya sukari hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani hivyo itahakikisha kwamba inaendelea kushirikiana bega kw began a wawekezaji wengine ili waweze kulima mashamba ya miwa amabyo yataweza kuleta fursa ya ajira kwa vijana pamoja na upatikanaji wa sukari kwa urahisi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kwamba kukamilika kwa kiwanda hicho kitaweza kutoa fusa za ajira kwa vijana na kuondokana na wimbi la umasikini huku akipongeza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kutoa ardhi kwa ajili ya uwekezaji huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania.
“Kwa kweli mimi kama mkuu wa Mkoa wa Pwani napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wetu mpendwa Dk. John Pombe Magufuli kwa kuweza kutoa ardhi hii kwa mwekezaji amabye ameweza kuonyesha nia dhabiti kwa kuanzisha mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari pamoja na shamba kwa ajili ya miwa hii itaweza kusaidia hata kwa wananchi wetu kupata fursa ya ajira,”alisema Ndikilo.
Pamoja na hayo Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba katika Mkoa wa Pwani kwa sasa kuna mazao mbali mbali ya biashara ambayo yanaweza kuliingizia Taifa kipato,ikiwemo kilimo cha zao la korosho, ufuta, pammba pamoja na kilimo cha miwa ambacho kwa sasa kimeanza kushika kasi katika Wilaya ya Bgamoyo hivyo kuwahimiza wakulima wengine wadogo wadogo wa zao hilo kutumia nafasi hiyo kuweza kujiingizia kipato.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Bakresa Group Abubakari Bhakhresa amesema maradi huo wa kiwanda hicho umegharimu kiasi cha dola bilioni 100 ambapo eneo hilo lote lina ukumbwa wa hekta elfu 10,ambapo wanatarajia kuajiri watu zaidi ya 1500 pindi mradi ukimamilika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania TADB Japhet Justin alisema kwamba lengo lao kubwa ni kuwasaidia wakulima kwa kuwawezesha fedha kwa ajili ya kilimo na kwamba tayari washatoa fedha kwa ajili ya kilimo.