WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa kijiji Langata kabla ya kuanza zoezi la kuchoma nyavu haramu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TADB Bw. Japhet Justine akizungumza na wavuvi kwenye soko la Deepsea Jijini Tanga
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akichoma nyavu haramu
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, amewataka wananchi
wanaofanya shughuli za uvuvi katika Bwawa la nyumba ya Mungu Wilayani
mwanga Mkoani Kilimanjaro kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano na
kukataa kabisa shughuli za uvuvi haramu.
Mpina ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo aliposhiriki katika kuteketeza
kiasi cha makokoro thelathini na nne (34)yani nyavu haramu,
zilizokamatwa na jeshi la police kwa kushirikiana na halmashauri ya
wilaya hiyo katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu katika
kijiji cha langata.
“Wizara peke yake haitaweza, Serikali peke yake haitaweza, kila siku
tunaambiwa kuhusu uvuvi haramu, nyavu mumenunua kwa gharama kubwa leo
zinaenda kuchomwa moto wakati ufike sasa shughuli za uvuvi haramu
zikome.” Alisisisza Mpina.
Aliendelea kusema wapo watu wanafikiria kuwa ikifika wakati wa uchaguzi
wataendelea na shughuli hizo na hawata kamatwa, alisema mtu yoyote
atakayefanya uvuvi haramu hata siku ya uchaguzi akiwa katika mstari wa
kupiga kura atakamatwa na sheria itachukua mkono wake.
“Hizi Rasilimali
za uvuvi zinatakiwa kulindwa usiku na mchana, rasilimali hizi ni za
kwenu sisi mumetupa jukumu la kuzilinda tu,na sisi viongozi wote
tutapita tuu ila hizi rasilimali zitabakia kuwa za kwenu” Alisema
Awali akiongea nakusikiliza malalamiko ya wafugaji katika Wilaya ya
Same, Waziri Mpina Alisema kuwa wafugaji wataendelea kusikilizwa na
kuwataka wataalam wa wizara ya mifugo na uvuvi kupitia team maalum ya
kutatua migogoro kushughulikia migogogoro inayowakabili wafugaji katika
wilaya za Same, Mwanga na Lushoto.
Waziri Mpina pia aliwataka wakulima na wafugaji kuitumia kwa faida Bank
ya Taifa ya Maendeleo ya kilimo katika kupata fursa za kuweza kuchukua
mikopo ya riba nafuu ili kuweza kuinua mitaji yao kwa mfano wavuvi
kununua na kutumia zana za kisasa za uvuvi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ndugu Japhet
Justine, alimuhakikishia Mhe. Waziri kuwa, Bank hiyo ipo tayari
kuwawezesha wafugaji na wavuvi kupitia vyama vya ushirika chini ya
usimamizi na udhamini wa wakurugenzi wa Halmashauri husika.