**********************************
Maofisa Wanandhimu na Wahasibu wa Jeshi la Polisi nchini wametakiwa kuongeza kasi katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali hususani katika faini za barabarani.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Christopher Kadio wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Wanadhimu na Wahasibu kutoka kutoka Makao Makuu ya Polisi, Mikoa na Vikosi vya Polisi Tanzania bara na Zanzibar kinachofanyika Shule ya Polisi Moshi.
FOOTAGE: CHRISTOPHER KADIO- Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Fedha na Lojistiki, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dhahiri Kidavashari amesema kikao hicho cha siku mbili kinalenga kuwasaidia watendaji wa Jeshi la Polisi kufanya kazi zao kwa weledi na kujifunza mifumo mipya ya malipo Serikalini ili kuboresha utoaji huduma kwa Askari na Raia kwa ujumla.
FOOTAGE: DCP DHAHIRI KIDAVASHARI- Kaimu Kamishna wa Fedha na Lojistiki.
Kikao hicho kinaongozwa na Kauli mbiu isemayo “UADILIFU KATIKA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA HUCHAGIZA MAENDELEO “